Alhamisi, 29 Septemba 2016

UTAFITI WA TWAWEZA UMEBAINI ASILIMIA 80 YA WANANCHI WANATAKA MAENDELEO NA SI SIASA.

ASILIMIA 80 ya Watanzania wamesema juhudi za maendeleo hazina budi kupewa kipaumbele baada ya uchaguzi na kukataa mikutano ya kisiasa ambayo wanadai hukwamisha shughuli za  maendeleo.

Taarifa ya utafiti huo iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaaam na Shirika la Utafiti la TWAWEZA ilisema kuwa utafiti huo umebeba maoni ya wananchi kuhusu  demokrasia, udikteta na maandamano nchini Tanzania.

Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa takwimu za muhtasari huo  zinatokana na na utafiti wa sauti za wananchi ikiwa ni moja ya programu za Twaweza.

Pia katika utafiti huo, wataalamu hao waliweza kubaini kuwa asilimia 49 ya wananchi wanakubaliana na kuzuiwa kwa mikutano ya vyama vya siasa kutokana na kwamba huvuruga umakini wa Serikali na Wananchi.

Katika suala la kumhusisha Rais Maguli na udikteta utafiti huo umebaini kuwa asilimia 58 ya Watanzania wanapinga uwepo wa udikteta katika serikali ya awamu ya Tano ya Rais John Magufuli.

Aidha utafiti huo wa Twaweza pia umebainisha kuwa asilimia 50 ya wananchi wamesema hakuna uwezekano wa wao kushiriki kwenye maandamano yoyote.

Kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kuzuia mikutano ya hadhara utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 60 wanamuunga mkono Rais katika kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa.

Utafiti huo wa Twaweza umekuja baada ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kujipatia pongezi nyingi kwa jitihada zake za kupambana na na vitendo vya rushwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni