Jumatatu, 19 Septemba 2016

WAZIRI MBARAWA AMEMTEUA DR MUSA MGWATU KUWA MTENDAJI MKUU WA TEMESA .




Dkt Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame M. Mbarawa(Mb), amemteua Dkt. Musa Mgwatu kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

. Mgwatu amechukua nafasi ya Mhandisi Marcellin Magesa  ambaye amepangiwa majukumu mengine  Wizarani.

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Mgwatu alikuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO).

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amemteua Bw. Masanja Kadogosa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa RAHCO.
            
Uteuzi huo unaanza mara moja.
                                         
                                             Imetolewa na
                                     Eng. Joseph M. Nyamhanga
                                           Katibu Mkuu (Ujenzi)
                     Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni