Septemba 10, Rais Dkt. John Pombe
Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza
nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Miongoni mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku
kuanzia jumatatu hadi Ijumaa.
Hudson Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuteua watangazaji
kushika nyadhifa mbalimbali kwani alimteua aliyekuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin
Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni