WANANCHI walioshuhudia tukio la kupatwa kwa jua Rujewa wilayani Mbarali mkoa Mbeya hofu yatanda kupatwa kwa ulemavu wa macho kutokana na kushuhudia tukio hilo pasipo miwani .
Wakizungumza na mtandao huu wa matukiodaimaBlog wananchi hao wamelalamikia utaratibu mbovu wa serikali ya mkoa wa Mbeya kupitia idara ya afya kushindwa kupeleka vifaa vya kutosha hasa miwani ya kuwezesha kushuhudia jua bila madhara
Amos Sanga na Amina Kyando walisema pamoja na kukesha kusubiri tukio hilo ila wameondoka eneo hilo bila kuona tukio hilo kutokana na hofu ya kupatwa ulemavu wa macho
Hivyo walisema moja kati ya miradi ambayo serikali inapaswa kuanzishwa eneo hilo ni pamoja na kituo cha afya maalum kwa ajili ya kutibu macho kutokana na wananchi wengi kushuhudia tukio hilo bila kinga.
Huku mamlaka ya hifadhi za Taifa (Tanapa) ikitumia tukio hilo kuanzisha lango maalum laUtalii kuingia hifadhi ya Taifa ya Ruaha lango la Ikoga na kutoa ofa kwa wanafunzi zaidi ya 100 Kutembelea hifadhi hiyo bure
Akizungumza katika tukio hilo afisa habari wa Tanapa Paschal Sherutete alisema kuwa tukio hilo limefungua fursa kubwa kwa watanzania kuendelea kupenda utalii wa ndani pia wao Tanapa kama njia ya kutangaza utalii wameona ni vema kufungua lango hilo.
Sherutete alisema tukio hilo la kupatwa kwa jua limeonyesha jinsi ambavyo watanzania wanavyopenda utalii na kuwa idadi ya wananchi waliofika kwenye tukio hilo ni ishara tosha kuwa suala hilo linawezekana.
Hata hivyo aliwataka watanzania kuendelea kutembelea hifadhi za Taifa badala ya kuwaachia wageni pekee.
Mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa chama cha waandishi wa habari za utalii na uwekezaji Tanzania ( Tataji) Felix Mwakyembe alisema kuwa tukio hilo limefungua utalii kwa mkoa wa Mbeya na Njombe na kuwa ni vema suala hilo kuendelezwa zaidi
Alisema kwa kuanza wao kama wanahabari wameanzisha chama cha utalii na uwekezaji hasa kuona kanda ya nyanda za juu kusini inapaa katika utalii na uwekezaji
Hata hivyo alisema wao ndio wamehamasisha zaidi tukio hilo na kumekuwa na mafanikio makubwa zaidi kuwa na wageni toka nje wengi
kuwa kupitia tukio hilo baadhi ya watalii toka nje wamepanga kutembelea eneo la Ihefu ambako ni miongoni mwa vyanzo vya maji vya Mto Ruaha mkuu na kutembelea hifadhi ya Ruaha
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala akizungumza na wananchi hao waliofika kushuhudia tukio hilo japo alisema mkoa wa Mbeya kupitia tukio hilo wanampango wa kulienzi eneo hilo kwa kujenga mradi wa kumbukumbu
Mwanasayansi Dr Noorali Siwaji ambae ni mhadhiri wa chuo kikuu Huria cha Tanzania alisema tukio hilo ni kazi nzuri inayofanywa na Wanasayansi nchini
Japo alisema kuwa tukio hilo ni watu kujifunza sayansi na kuwa kupatwa huko kwa jua ni matukio ambayo hutokea Mara chache zaidi na kuwa wananchi wameshuhudia kupatwa kwa jua kwa mwonekano wa Pete.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni