Jumapili, 11 Septemba 2016

MKUU WA MKOA WA TANGA MARTINE SHIGELLA ATEMBELEA MAMLAKA YA MAPATO TANGA.

 Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella pamoja na katibu Tawala Mkoa Zena Said walipotembelea Mamlaka ya Mapato kuona utendaji kazi wa Mamlaka hiyo na changamoto zinanzo wakabili.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa  wa Tanga Salehe Byalugaba akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella wanavyofanya kazi na kukabiliana na changamoto zilizopo hapa Mkoani. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga pamoja na Tatibu Tawala Mkoa wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mhasibu wa Mkoa wa Mamlaka ya Mapato Audifas Shao ambaye hayupo kwenye picha
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato  Tanga wakisikiliza kwa makini Taarifa inayotolewa na Meneja wa Mapato Mkoa Salehe Byalugaba kwa Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga  Martin Shigella akizungumza na Wafanyakazi wa sekta tofauti wa Mamlaka ya Mapato Mkoani Tanga.

HABARI:
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella amefanya ziara ya katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Mkoani Tanga na kusikia mafanikio ya mamala kwa mwaka 2014 /2015 na mipango iliyopo ukuelekea Mwaka wa 2020.
 
Akitoa taarifa fupi Meneja wa Mamlaka hiyo Salehe Byalugaba  amesema Mamlaka inakabiliwa na uchakavu wa vitendea kazi ambavyo ndiyo msingi mkuu wa kazi kwani kwa sasa mkoa wa Tanga umekuwa  Bandari bubu  nyingi zinazo pitisha Magendo kwa wingi  kupitia Bahari ya Hindi.

Byalugaba amesema wafanyakazi wa mamlaka ya mapato wanayo hali ya kufanya kazi endapo wataweza kupata vitendea kazi kama Gari na Boti kwajili ya  kuzunguukia maeneo mbalimbali yanayoingizia bidhaa kinyemela iki ni pamoja na eneo la  Baharini.
Pia Meneja amemweleza mkuu wa mkoa mpango uliowekwa na  Mamlaka hiyo wa kutoa elimu wa wateja ya matumizi mashine ili kuzuia upotevu wa Mapato ya Taifa yanayokusanywa na mamlaka ya Mapato (TRA).

“Kwa sasa tumejipanga kutoa elimu kwa wananchi wote umuhimu wa pato la taifa kwa yeyote atakaye nunua bidhaa adai lisiti na muuzaji atoe lisiti kwa wateja wake” amesema Byalugaba

“Nakwasasa tumetoa barua kwa wamiliki wote wa vituo vya mafuta mkaoni hapa ifikapo mwishoni mwa mwezi  Septemba vituo vyote viwe vimefunga mashine na kuzitumia” amesema Byalugaba

Hata hivyo Byalugaba amewataka wananchi na wakazi wa maeneo ya jirani na Bahari kuacha kuwapokea na kuwaifadhia bidhaa wafanyabiashara ya magendo wanaofanya biashara hiyo kwani kwa sasa siyo biashara inayofaa tunapoteza Mapato mengi kwa njia ya panya na wanaofanya biashara hiyo waache haraka.
  
kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella amewapongeza wafanyakazi wa mamlaka ya Mapato kwa kujitumaa kwao kuakikisha pato la Taifa halipotei na kuweka mikakati ya kupambana na mianya ya upotevu wa Mapato.

“Tangu nifike mkoa wa Tanga sijapata malalamiko ya utenda kazi wa mtumishi hata mmoja wa mamlaka ya mapato naomba mwendelee kufanya kazi tena kwa uadilifu huohuo”alisema  Shigella.

“nitajitahidi kuhakikisha changamoto za vitendea kazi zinatatuliwa ili muweze kufanya kazi bila shida yoyote ili tuweze kufikia malengo tuliyo wekewa kitaifa”alisema Shigella.

Pia mkuu wa mkoa amewataka wananchi wote kushirikiana kupambana na kutoa taarifa ya magendo  kwani kuingia kwa bidhaa au kutoka kwa bidhaa bila kulipiwa ushuru ni hasara kwa Taifa.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni