Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, leo tarehe 21 Septemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi
ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Prof. Hasa Mlawa kuanzia leo.
Pamoja na kutengua uteuzi wa Prof. Hasa Mlawa, Rais Magufuli
amevunja Bodi ya Udhamini ya Mfuko huo.
Uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Udhamini ya LAPF
utafanywa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni