Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa
kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba
taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.
Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa
kwenye taharuki. Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya
nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa
ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano
mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.
Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya
kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu
nchini.
Imetolewa
na
Ofisi
ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni