Jumatatu, 12 Septemba 2016

RAIS MAGUFULI AHAIRISHA SAFARI YAKE YA ZAMBIA SABABU YA JANGA LA TETEMEKO.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara yake  ya siku tatu Nchini Zambia  ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ahudhurie Sherehe  za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu, ili aweze kushughulikia tatizo laTetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16, mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa  zimebomoka Mkoania Kagera

Kufuatia kuahirishwa kwa ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Kumuwakilisha katika Sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika kesho tarehe 13 Septemba, 2016 katika jiji la Lusaka


                            Jaffar Haniu
               Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
                           Dar es salaam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni