Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Mtanga Nnour, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shlingi milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla, ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa. Nyuma ni mkuu wa fedha, Pietre Jaggar.
Mhasibu wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Emmanuel Jonas, akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mkuu wa fedha kiwanda cha saruji cha Simba Cement, Pieter Jaggar, akimabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa, kulia ni meneja usambazaji na ugawaji, Samwel Shoo, nyuma kulia ni Afisa Uhusiano , Nour Mtanga na mkuu wa Idara ya Rasilimawatu, Diana Malambugi.
HABARI KAMILI
KIWANDA Cha Saruji Cha
Simba Cement kilichopo Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya
Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya
milioni 4.8 kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Akizungumza katika wa halfa
fupi ya makabidhiano , Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha
Simba Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza
changamoto za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.
Malambugi alisema msaada huo
utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama
ilivyokusudiwa na kuiagiza kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika
ipasavyo.
‘Mifuko hii ya saruji
itapunguza changamoto inayoikabili shule ikiwemo vyumba vya madarasa na ujenzi
wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii yakusaidia elimu” alisema Malambugi.
Alimtaka mwalimu na kamati yake
ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo
kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu
zikiwemo kuondosha uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.
Kwa upande wake, mwalimu mkuu
wa shule ya Ilboru sekondari school,
Julias Shulla, alishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo
utatumika kama ilivyoombwa.
Shulla alisema shule yake
inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja
uhaba wa vifaa vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.
Pia alisema mifuko hiyo
itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto
ambazo shule yake inakabiliana nazo kwa
msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa shule yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni