Jumamosi, 1 Oktoba 2016

BONANZA LA WATUMISHI WA UMMA TANGA KUSHIRIKISHA VIONGOZI MBALIMBALI WA MKOA TANGA.




 Bonanza la taasisi za umma limefanyika hii leo kwa mwitikio mkubwa wa watumishi wa Umma na kufunguliwa na Katibu Kawala Mkoa wa Tanga Zena Ahamed Said katika viwanja vya shule ya secondary POPATLAL (Picha juu Katibu Tawala Mkoa akipiga mpila kufungua michezo)

Michezo mbalimbali ilichezwa ikiwa ni kuvuta kamba timu ya Mamlaka ya Bandari Tanga waliopambana na timu ya Mahakama Tanga na timu ya Bandari kuibuka mshindi kwa kuwaburuza timu ya Mahakama.  
 Mpambano  kati ya timu ya Katibu Tawala mkoa Tanga na timu ya Mamlaka ya  Bandari Tanga upamde wa wanawake, ambapo timu ya Katibu Tawala Mkoa imewaburuza timu ya Bandari.



Mchezo wa karata nao haukuachwa nyuma ikipambana vikali timu ya Mahakama na timu ya Mamlaka ya Bandari na kutoka sare kwa 2 -2  kufungana 
Sambamba na michezo kulikuwa na zoezi la kuchangia Damu kwa hiyari ambapo Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Zena Ahamed Said aliongoza wanamichezo kuchangia Damu kwa hiyari  ili kuwasaidia wagonjwa waliopo katika Hospitali mbalimbali mkoani hapa.


Naye Katibu Tawala Wilaya ya Tanga Faidha Salimu akijumuika na wanamichezo  katika zoezi la kuchangia damu kwa hiyari. 
Baadhi ya washiriki wa Bonanza wakiongonzwa na Afisa Michezo jiji la Tanga Norbet  Achiula, Judith Mzia  na Tabu Kassim wakichangia damu kwa hiyari.
HABARI
Michezo ni tiba michezo ni furaha michezo ni afya ni leo imedhiilika katika Mkoa wa Tanga kwenye bonanza lililoandaliwa na ofisi ya katibu tawala mkoa wa Tanga.

Akizungumza wakati wa ufungunzi wa bonanza hilo Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Zena  Ahamed Said amesema wanajipanga angalau kufanya bonanza hili kila baada ya miezi mitatu ili kuweka safi afya za watumishi wa Umma.

Zena amesema kwa michezo hii watumishi wamejuana na kushirikiana katika michezo mbalimbali hivyo upo umuhimu wa michezo kwa watumishi wa Umma

Pia amewataka watumishi wa Umma kujitokeza mara watakapo andaa bonanza jingine kwa ustawi wa afya na akili.

Kwa  upande wake mratibu wa bonanza hili Jacob Kingazi amesema mwitikio wa ushiriki umekuwa ni mkubwa sana  na mzuri kwani nakuwataka watumishi kushiriki katika mabonanza mbalimbali kwani yanasaidi kujuana na kuweka afya vizuri.

kingazi amewataka wadau mbalimbali kujitoa kusaidia pale wanapoandaa Bonanza kwani kwa upande wa watumishi linawasaidia kufahamiana na kushirikiana. 

Naye Mganga  mkuu wa mkoa wa Tanga Asha Mahita amewashukuru wote waliojitolea Damu amesema unapotoa damu unaokoa maisha ya mtu mwingine mwenye uhitaji wa damu.

Mahita amesema zoezi la uchangiaji wa damu kwa hiyari ni endelevu kwahiyo watu wanakaribisha wajitokeze kuchangia damu katika Hospital Bombo.      








 







 



 





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni