Mkurugenzi mkuu
wa Mamlaka ya usafiri wa baharini zanzibari Suleiman Makame akizungumza na Waandishi
wa Habari mkoani Tanga hapo jana.
Mwandishi wa Habari Gabriel Kapembe (TBC) akiuliza swali kwa viongozi wa Ulinzi na Usalama Baharini.
Serikali inatarajia kuzindua mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa katika eneo la bahari ikiwa ni njia ya kukabiliana na changamoto itakayo sababishwa na ongezeko la meli kubwa zitakazo kutiananga katika bandari za Tanzania bara na Zanzibari.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (Simatra),Captain Mussa Mandia alisema hayo jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia maadhimisho ya wiki ya bahari duniani yanayofanyika kitaifa jijini Tanga.
Mandia alisema Serikali ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa mpango maalumu wa kupambana na uchafuzi wa bahari (NMOSCRP) ambao utaviwezesha vyombo vinavyohusika na bahari kuhakikisha mazingira ya bahari hayachafuliwi.
“Serikali ya awamu ya tano imeazimia kuendesha uvuvi wa kisasa katika bahari ya hindi na maziwa yake kwa maana hiyo ni wazi kwamba zitakuja meli kubwa kuvua,kama hatutaweka mpango wa kudhibiti uchafuzi bahari yetu itachafuliwa sana”alisema Mandia.
Alisema uzinduzi wa mpango huo utafanyika wiki hii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya bahari dunia ambapo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzui na mawasilianoProfesa Makame Mbarawa atakuwa mgeni rasmi.
Selemani Musa Makame kutoka Mamlaka ya meli Zanzibar (ZMA),alisema katika uzinduzi huo,Waziri wa Biashara ,Amina Salum Ali ataiwakilisha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika uzinduzi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni