Watoa mada kutoka mfuko wa hifadhi ya Taifa ya PSPF wakimsikiliza mgeni rasm
Wadau na wanachama wa Hifadhi ya Taifa ya PSPF wakiwa kwenye mkutano wa uliofanyika jana Jijini Tanga.
Serikali imeombwa kuhakikisha kila mtanzania yeyote ambaye ana umri wa
miaka 18 na kuendelea awe ameajiriwa au amejiajiri kujiunga na huduma
za mifuko ya hifadhi ya jamii ili waweze kunufaika na mafao mbalimbali
yatolewayo na mifuko hiyo.
Rai hiyo imetolewa na Afisa masoko mfuko wa pensheni wa PSPF Magira
Werema wakati alipokuwa kwenye mkutano na wadau wa mfuko huo ambao ni
wananchama na wasio wananchama ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha
wajasiriamali Mkoani Tanga.
Watanzania wametakiwa kujiunga na mifuko hiyo ili kuweza kujipatia
fursa mbalimbali zitokanazo na mifuko hiyo sambamba na kujua huduma
zinazotolewa na mifuko kwa faida yao.
Werema alisema lengo la kufanya mkutano huo Mkoani Tanga ni kwa ajili
ya kutoa elimu juu ya hifadhi ya jamii ili watanzania wengi waweze
kuelewa umuhimu wa hifadhi za jamii na huduma zinazotolewa na shughuli
wanazoendesha ni nanma gani wao kama wanachama wa PSPF wanaweza
kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.
Alisema mbali na hayo wananchama wataweza kufahamu shughuli
wanazoziendesha zitaweza kuwasaidia kwa namna gani katika kuwaletea
maendeleo sanjari na kuboresha hali za maisha za watanzania walio
wengi.
Werema aliyataja baadhi ya mafao yanayotolewa na mfuko wa PSPF kuwa
ni pamoja na fao la uzazi, fao la kujitoa, mkopo wa elimu, mkopo wa
mwajiriwa mpya, mkopo wa viwanja, mkopo wa nyumba, mkopo wa fedha
taslimu, mkopo kwa wastaafu wenye masharti nafuu, fao la
ulemavu,matibabu na mirathi, fao la kufukuzwa au kuachishwa kazi, fao
la wajasiriamali, pamoja na fao la uzeeni.
“Ombi letu kwenu wananchama kuwa mabalozi wazuri ili PSPF iendelee
kuwa chaguo namba moja kwa waajiri wapya Nchini kwani PSPF itazidi
kuwa pamoja nawe kwa kuendelea kubuni huduma mbalimbali zitakazoendana
na mahitaji ya wakati uliopo sasa na baadaye,”alisisitiza Werema.
Alisema baadhi ya mafanikio waliyoyapata ni pamoja na kuendelea kupata
wanachama kwa wingi mbali na ushindani mkubwa wa mifuko uliopo,
michango ya wananchama imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, kukuza
mahusiano na waajiri na wanachama pamoja na kuwekeza kwenye mifumo ya
habari na mawasiliano ambayo imeongeza ufanisi katika kutoa huduma.
Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo werema alisema ni
kukosekana kwa nyaraka muhimu wakati wa ukokotoaji wa mafao hivyo
kusababisha ucheleweshwaji usio wa lazima pamoja na kuwepo vishoka na
uwepo wa nyaraka zenye taarifa zinazikinzana kama vile majina, tarehe
za kuzaliwa na tarehe za ajira.
Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo wamejipanga kutoa elimu
zaidi kwa waajiri, wananchama na wananchi kwa ujumla ili kuhakikisha
kuwa matatizo ya kukosekana kwa nyaraka na upotoshwaji wa kupata
huduma ambazo ni haki ya mteja zinafanyiwa kazi ipasavyo.
Awali akifungua mkutano huo, Katibu tawala Mkoa wa Tanga Zena Saidy
alisema ni vyema watanzania wakajiunga na mifuko hiyo ili kazi zao
ziweze kuonekana zaidi ikiwa ni pamoja na kila mmoja kutimiza wajibu
wake ipasavyo katika utendaji wake ili kuongeza ufanisi kwa maslahi ya
jamii na taifa kwa ujumla.
Sambamba ha hayo Zena aliwataka PSPF kufanya kazi kwa weledi na
nidhamu kwa kuzingatia dira na dhima za uchapaji kazi pamoja na utoaji
wa huduma bora kwa wananchama wake.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni