JESHI la polisi kanda maalum Dar es salaam, limeahidi
kuwachukulia hatua kali wananchi wanaotumia vibaya simu za dharura, zenye namba
111 na 112.
Simon Sirro, kamishina wa jeshi la polisi amesema kuwa watu
wamekuwa wakipiga simu hizo na kutoa taarifa za uongo au kupiga simu na kisha
kuwapa watoto wadogo waongee.
“Polisi tutawafuatilia wote
kupitia mitandao yetu general packet radio service (gprs),inayoonyesha maeneo
walipo na simu wanazotumia ili kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za
kisheria. haiwezekani mtu apige simu halafu baada ya simu kopokelewa anaweka
muziki,” amesema.
Kamanda Sirro amesema ni vyema wananchi wakaacha mzaha na
matumizi ya namba hiyo ya jeshi la polisi kwani kwa kufanya hivyo inapunguza
morali ya askari wa jeshi hilo kufanya kazi kwa kujituma.
“Wananchi wote watumie simu zetu
kutoa taarifa zenye ukweli na zitafanyiwa kazi kwa wakati, wawasiliane na sisi
pale wanapoona viashiria vya uhalifu ama tukio lolote linaloleta uvunjifu wa
amani na siyo kupiga simu na kufanya mzaha,”
amesema Sirro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni