Uongozi wa mkoa wa Tanga ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa Martine Shigella wakiwasili katika Ofisi za Mamlaka ya Bandari kwa ziara yakuona utendaji kazi wa Bandari hiyo.
Mhasibu wa Mamlaka ya Bandari pamoja na Katibu Tawala Mkoa na Mkuu wa Mkoa wakatikati akijiandaa kupanda meli.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Henry Arika akiteta neno na Afisa Habari Mamlaka ya Bandari Bi Moni katikati nyuma ni waandishi wakiwa kwenye ziara.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akipanda Meli ndogo iitwayo spana kondo na kupokewa na capten.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga kushoto akizungumza wakati wa safari ya ziara
yake aliyoifanya katika Bandari ya meli kubwa zinazotiananga ndani ya
Bahari ya Hindi.
Mkuu wa mkoa wa Tanga akishuka kwenye Meli ndogo ya Mamlaka ya Bandari tayari kuingia kwenye meri kubwa iitwayo TR CROWN kutoka nchini America iliyoleta shehena ya kichele.Mkuu wa Mkoa wa Tanga akipakia kwenye meli hiyo ya TR CROWN
Mkuu wa Mkoa wa Tanga akirudi taratibu baada ya kutoka ziara ya kwenye meli kubwa iliyotia nanga katika Bandari ya Tanga.
HABARI
KUFUNGWA kwa viwanda na uchakavu wa vifaa vya bandari ya Tanga
na upungufu wa uzalishaji wa mazao ya biashara kama vile katani, kahawa,na
mazao ya misitu imeathiri kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha shehena
inayopita bandari ya Tanga.
Alisema hayo Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Henry Arika wakati akitoa Taarifa fupi ya utendaji wa
mamlaka hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella alipofanya ziara yake
7septemba,2016 katika Bandarini hiyo.
Arika alisema Mamlaka ya Bandari imejipanga kutoa huduma
bora kwa wateja wake wa ndani na nje ya nchi kwa masaa 24 ilikuhakikisha
wanafikia malengo walio jiwekea katika kutoa huduma bora na umakini kwa wateja
wanao tumia bandari hiyo.
“Kwa sasa zipo changamoto zinazo turudisha nyuma katika
kufanyaji kazi ikiwa ni pamoja na Mamlaka tunazoshirikiananazo kufanya kazi
kushindwa kufanya kazi kwa masaa 24, kuendana na kasi waliyo nayo wafanyakazi
wa mamlaka ya Bandari ya kupokea na kusafirisha mizigo”Alisema Arika .
Hata hivyo kaimu meneja wa mamlaka ya bandari amemwomba Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kuzungumza na Mamlaka nyingine ikiwemo Mamlaka
ya Mapato, Benk ya CRDB na NMB kuona jinsi watakavyoweza kufanya kazi kwa masaa
24 kuendana na wafanyakazi wa Bandari ili kukwepa kurundika shehena kwa muda
mrefu na kufanya mizigo kutoka kwa wakati.
Pia ameshukuru msaada wa kimaendeleo walioupokea kutoka kwa Serikali
ya watu wa China Kwa kuweze kuwajengea wa skan ambayo itawasaidia katika
ukaguzi wa mizigo inayo toka na kuingi katika bandari ya Tanga ambayo itasaidia
bandali kuongeza mapato ya ndani na kukuza uchumi wa taifa.
Naye mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella baada ya kufanya
ziara yake hiyo nakujionea utendaji wa bandari ya Tanga na kuridhishwa kwa
utendaji kazi wa bandari kwa uongozi wafanyakazi pamoja na vibarua Bandarini
hapo.
Shigella amewataka wananchi wa kanda ya kaskazini kanda ya
ziwa na nchi jirani zote na kuitumia kusafirisha mzigo kwa bandari ya Tanga
kwani kwa sasa Mkoa utahakikisha huduma zote zinapatikana bandarini kwa ubora
na wakati.
“Bandari ya Tanga inakina kirefu na inauwezo wakupokea meli
kubwa na vifaa vyakutosha wafanya biashara ndani na nje ya nchi karibuni
mpitishe bidhaa zenu kwenye Bandarini ya Tanga”. Alisema Shigella.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni