SERIKALI
ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la
mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi
bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Uamuzi
huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika
tarehe 29 Septemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Taarifa
ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote
kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Amesema
ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5
ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa
Tanzania.
Mradi
huo mkubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa
kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya
Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda.
Mhe.
Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443
linatarajiwa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku ambapo kila pipa
litaliingizia taifa Dola za Marekani 12.2.
Amebainisha
kuwa pamoja na kusafirisha mafuta ya kutoka nchini Uganda bomba hilo
pia linatarajiwa kusafirisha mafutakutoka nchi nyingine zaJ amhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na Sudani Kusini ambazo zimeonesha nia ya
kusafirisha mafuta yao kupitia bandari ya Tanga.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ametaja faida nyingine ambazo Tanzania itazipata
kutoka na namradi huo kuwa ni kupatika na kwa ajira zaidi ya 15,000
wakati wa ujenzi na ajira 2,000 baadaya ujenzi kukamilika, kuimarika kwa
mahusiano ya kidiplomasia, kukuza biashara katika ukanda wa kaskazini
mwa Tanzania, kampuni za ujenziza Tanzania kupata kazi za ujenzi.
Aidha,
amesema Tanzania inatarajia kunufaika zaidi kwa kutumia bomba hilo
kupitisha mafuta yanayotarajiwa kupatikana katika maeneo ya ziwa
Tanganyika na Ziwa Eyasi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, SEPTEMBA 28, 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni