CHAMA cha Mapinduzi, CCM, wilaya
ya Arusha, kimempongeza Rais Dakta John Magufuli, kwa kazi
anzozifanya tokea achaguliwe kushika wadhifa huo Oktoba 2015 na kuonyesha
dhamira yake ya kweli ya kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi, upendeleo katika
kuharakisha maendeleo ya taifa.
Tamko la kamati ya siasa ya
halmashauri kuu ya CCNM, wilaya lililotolewa na Katibu mwenezi wa Wilaya ya
Arusha, Jasper Kishumbua, limesema kwa kipindi kifupi rais Magufuli,
amerejesha heshima na nidhamu kwa watumishi na watendaji wa serikali.
Kuhusu ahadi, za rais, tamko hilo
limesema kuwa rais Magufuli ambae pia ni mwenmyekiti wa Chama cha Mapinduzi,
amekuwa ni kiongozi wa aina yake kwa kutekeleza ahadi mbalimbali alizozitoa
wakati wa kampeni Amezitaja baadhi ya ahadi hizo kuwa ni pamoja na kununuliwa
ndege mpya mbili ambazo zimeshawasili nakuzinduliwa rasmi jana ,katika kipindi
chake kifupi cha uongozi tayari ameishaipatia mahakama kuu fedha za
kuendeshea shughuli zake ikiwa ni hatua ya kuuboresha muhimili huo.
Mbali na rais, pia kamati ya siasa
ya halmashauri kuu ya wilaya, imewapongeza mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo na mkuu wa wilaya ya Arusha, Fabiani Gabriel Daqarro, kwa
kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kutokana na kuwa msitari wa mbele
kutatua kero za wananchi jijini Arusha.
Miongoni mwa kero hizo ni pamoja
na kuwezesha kulipwa malimbikizo ya madai ya walimu 700 ,ambao wamelipwa
shilingi milioni 169.
Amesema fedha hizo zimelipwa
kutokana na agizo la mkuu wa mkoa, Mrisho Gambo, alilolitoa kwenye kikao cha
walimu wa shule Septemba 19 mwaka huu kilichofanyika ukumbi wa mikutano ya
kimataifa, AICC mjini Arusha.
Tamko limesema agizo hilo
limetekelezwa ndaniya siku tano likisimamiwa na mkuu wa wilaya ya Arusha,
Daqarro.
Tamko limesema mkuu wa mkoa
ameonekana kukerwa na matumizi yasiyokuwa ya msingi ambapo aliagiza
kubadilishwa kwa matumizi ya fedha zilizokuwa zikitumika kuwalipa
madiwani posho.
Aidha tamko hilo limelaani na
kukemea kwa nguvu tamko lililotolewa na meya wa jiji la Arusha,Karisti Lazaro,
lililojaa upotoshaji na uchonganishi kati ya wananchi na serikali
Septemba 20 mwaka huu la mkuu wa mkoa kubadilisha malipo ya posho ya madiwani
na badala yake fedha hizo kutumika kuwalipa walimu madeniyao.
Aidha Kamati hiyo ya siasa
imefuatilia madai ya Meya, ya kuhusu watoto waliozuiwa kwenda shule kwa
madai wakuu wa shule walienda kwenye kikao na mkuu wa shule hivyo hawakupata
masomo siku hiyo na kugundua kuwa ni tuhuma ambazo hazina ukweli.
Tamko hilo limewataka viongozi
kuacha kutoa matamko ya kiuanaharakati ambayo yanalenga kuwapatia umaarufu na
kuwapotosha wananchi na badala yake watoe matamko yanayohamasisha maendeleo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni