Jumatano, 7 Septemba 2016

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJI LA TANGA YAPATA TUZO KWA MARA YA TATU MFULULIZO YA UTOAJI HUDUMA BORA ZA MAJI NCHINI.

 MKUU WA MKOA WA TANGA MARTINE SHIGELA AKIPOKEA CHETI YA ISO NA KUMKABIDHI MWENYEKITI WA BODI YA TANGA UWASA.
 MWENYEKITI WA BODI YA TANGA UWASA AKIMKABIDHI TUZO MKURUGENZI MTENDAJI  MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA.



 MKUU WA MKOA WA TANGA MARTINE SHIGELA AKITEMBELEA NA KUONA JINSI KAZI ZA KUTIBU MAJI ZINAVYO ENDESHWA NA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJI LA TANGA.


MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA INJ. JOSHUA MGEYEKWA AKIMKABIDHI MKUU WA MKOA WA TANGA ZAWADI.
MWENYEKITI WA BODI ILIYOISHA MUDA NA MWENYEKITI MTEULE WA BODI MPYA YA TANGA UWASA BWANA SHAMTE.
 BAADHI YA WAFANYAKAZI WA TANGA UWASA.

WADAU WALIOFIKA KUSHUHUDIA TUZO YA TANGA UWASA.

HABARI KAMILI.


Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jiji la Tanga imezindua bodi mpya ya wakurugezi ya Tanga Uwasa na kupokea Tuzo ya Ubora wa kimataifa kupitia hati ya ISO 90012015 na kupokea Leseni daraja la kwanza ya EWURA kwa kuwa mamlaka Bora ya huduma Majisafi na usafi wa mazingira nchini kwa mwaka wa 2014/2015.

Hafra hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela, Mkurugenzi wa Ewura Felix Ngalamgosi Bodi ya Tanga Uwasa iliyomaliza muda wake na Bodi mpya iliyokabidhiwa madaraka Wadau na Watumiaji wa Maji wa Jiji la Tanga.

Katika hafra hiyo mkuu wa mkoa wa Tanga akiwamgeni rasmi amezitaka taasisi zote zinazo daiwa na mamlaka kulipa madeni yao yote ili kuifanya mamlaka ya majisafi iweze kumudu kujiendesha katika shughuli zake.

“ninaziomba Taasisi zote zinazodaiwa na Mamlaka ya Maji kulipa madeni yao yote nami naahidi kuzifwatilia kuhakikisha wanalipa kwa wakati bila kuzembea” alisema Shigela.  

Pia Shigela ametoa rahi kwa wananchi kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji na na kulinda maji yasipotee bila sababu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Inj. Joshua Mgeyekwa amesema sio kazi rahisi kwa miaka mitatu kukamata daraja la kwanza kwa utoaji huduma Bora Nchini ni kwa sababu ya ushurikiano tulionao uongozi na wafanyakazi pamoja na wadau  Watumiaji Maji Jijini Tanga.

Mgeyekwa amewataka wafanyakazi wa Tanga uwasa wasirudi nyuma wawe na hari hiyohiyo ya kuchapa kazi ili asitokee wa wakuwanyang’a nafasi hii na kujitahidi kuwa wa kimataifa zaidi.

Hata hivyo Inj. Mgeyekwa amewakaribisha mamlaka nyingine zote Nchini kuja kujifunza kutoka kwao jinsi walivyoweza kuendesha na wanavyopanga mipango ya ufanisi.  
    
“tunakaribisha mamlaka zinazopenda kujifunza kwetu kwani nasi tulijifunza kwa mamlaka zawenzetu na kuboresha na kufika hapa tulipo. Alisema Inj. Mgeyekwa.

Mgeyekwa amesema mamlaka inakabiriana na changamoto ya maji taka katika jiji hili la Tanga kutokana na uchakavu wa mabomba yalaliyopo na mikakati iliyopo kwa mwaka 2016/2020 ni kuhakikisha mabomba yote chakavu yanafumuliwa na kufungwa mabomba mapya.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni