Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Milapwa akizungumza na wafanyakazi pamoja na wadau wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Tanga Uwasa)
Meneja wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mzingira jijini Tanga (Tanga Uwasa) akizungumza na wadau wa Mamlaka hiyo kwenye kikao cha pamoja.
Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga Uwasa Haika Ndalama akitoa ufafanuzi wa jambo kwenye kikao na wadau.
Afisa Mahusiano wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dora Killo akitoa elimu katika mkutano walio uandaa.
TANGA.
Mamlaka
ya maji safi na usafi wa mazingira (Tanga Uwasa) jijini Tanga imetakiwa
kujipanga ili kuhakikisha inaboresha huduma ya sekta ya majisafi na majitaka
mjini Tanga.
Hayo
yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Milapwa katika ufunguzi wa mkutano
wa wafanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na wadau wa maji pamoja na madiwani wa
wilaya ya Tanga katika ukumbi wa Veta mkoani hapa.
Milapwa
alisema Mamlaka ya maji safi ijipange kutoa haki kwa wateja wake na kusikiliza
ushauri wa wadau wa maji kwa kufanya hivyo itakuwa imeondoa mapungufu na
kuboresha huduma kwa wahitaji wake.
Naye
Meneja wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira (Tanga Uwasa) jijini Tanga
Mohamed Pima alisema wamejipanga kuhakisha huduma ya maji safi na salama
yanatosheleza kwa wakazi wa jiji la Tanga na pembezoni mwa jiji hili kwa
asilimia 96.9.
Pima
alisema Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jiji la Tanga inatoa huduma
ya kuunganisha maji ndani ya siku saba tu na sio zaidi kwa wale wateja wapya
kwa huduma bora na yaharaka ni Tanga Uwasa.
Pia
Katibu Tawala mkoa wa Tanga Zena Said na mjumbe wa bodi ya Tanga Uwasa aliiomba
Tanga uwasa kuwasaidia wateja kwa kuwapatia mafundi bora wa kujenga mashimo ya
kuhifadhia maji taka ili kuepuka ujenzi olela na usio na ubora.
Zena
alisema majitaka ni tatizo na ujenzi wa mashimo yasiyo na kiwango yanayosababisha
kuvuja na kusambaa kwa maji taka mitahani na kuwanyima raha wateja.
Aliutaka
uongozi kuwasaidia wananchi kupata mafundi wenye ubora wa kujenga miundo mbinu
ya maji taka katika nyumba zao.
Kwa upande
wake Meya wa jiji la Tanga na Diwani wa Nguvumali Selebose Mustapha aliuomba
uongozi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kujitahidi kuweka vituo
vya kutolea malalamiko katika maeneo ya karibu na wananchi kwani kwa sasa jiji linakuwa
na uhitaji wa huduma majisafi ni mkubwa
.
Selebose
aliwataka wafanyakazi wa Tanga Uwasa kupitia mitaani mara kwa mara katika
maeneo korofi ya mabomba ya maji taka ili kukabiliana nazo na kufanya kuendelea
kuwa mamlaka bora kwa kutoa huduma maeneo yote na kuondoa kero za wananchi.
Kaimu
mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya
majisafi na Uasfi wa mazingira(Tanga Uwasa) Haika Ndalama alisema kero zote
zilizotolewa na ushauri wote wao kama Mamlaka watazichukuwa na kuzifanyia kazi
haraka iwezekanavyo.
Ndalama
alisema ili Mamlaka iweze kufanikiwa kujiendesha wateja wanatakiwa walipe bili
kwa wakati na kupitia Bank ya CRDB au NMB au M-pesa na Tigo pesa kwani kwasasa
Mamlaka haipokei pesa tasilm.
Alisema
wafanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira wamejipanga kutoa
huduma kwa kushirikiana na wananchi ili kuwafikia wote kwa huduma iliyo bora
zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni