Mamlaka nchini Tanzania imetaka madereva wanane waliotekwa nyara nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC waachiwe huru.
Jumatano wiki hii, waasi wa kundi la
Mai Mai walio nchini DRC walichoma moto malori 8 kutoka Tanzania na mengine 4
kutoka Kenya na kuwateka madereva wa malori hayo katika eneo la Namoya mkoani
Kivu.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje
nchini DRC Bi. Mindi Kasiga amesema, serikali za Tanzania na DRC zinajitahidi
kuhakikisha kuwa mateka hao wanaachiwa huru wakiwa salama na kurudishwa
Tanzania.
Mwaka jana mashehe wanane kutoka
Tanzania waliotekwa nchini DRC walifanikiwa kuokolewa kutokana na juhudi za
pamoja za serikali za nchi hizo mbili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni