Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa
kukamatwa na polisi wakiwa na zana mbalimbali ambazo hutumiwa na vyombo vya
ulinzi zikiwamo silaha za vita na sare za polisi.
Vitu hivyo vinadaiwa kutumiwa na watu hao
kufanya ujambazi.Inadaiwa kwamba watu hao ni wale waliovamia na
kuiba fedha katika jengo la Sophia House lililopo Keko Dar es Salam
wakiwa wamevaa sare za polisi na kutumia gari ya Noah.
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba
watu hao ni pamoja na mwanamke mmoja aliyekamatiwa Bunju
katika Manispaa ya Kinondoni ambako vilikutwa vitu vyote vilivyoporwa na
wanaume wawili waliokamatiwa Mbagala Manispaa ya
Temeke, Dar es Salaam.
Chanzo hicho kilieleza kwamba silaha zilizokamatwa ni
pamoja na bunduki tatu za SMG na risasi zake 260, bastola 16 na risasi zake
526, panga moja na michimbiko mitatu ya kung’olea mageti..
Vitu vingine ni pingu za chuma 45 na tatu za
plastiki, ‘radio call’ 12 , kamera ya CCTV moja, gari moja ya
Noah, sare ya polisi jozi moja, ‘pump action tatu na mkasi mmoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni