Tanga bado wawekezaji wengi wa viwanda hivyo wanalalamikia changamoto za uhaba wa nishati ya umeme pamoja na miundombinu ya reli.
Malalamiko hayo yametolewa na Mkurungenzi Mtendaji wa kiwanda cha
kuzalisha Saruji cha Sungura,Fauzi Tamimu Wakati akiongea
kuhusu changamoto za ukuaji wa sekta hiyo katikia mkoa huo.
Alisema kuwa iwapo huduma ya umeme itaweza kuimarishwa na kuwa ya
uhakikia wawekezaji wengi wataweza kuja kuwekeza katika mkoa Tanga kwani unamalighafi nyingi kwa ajili ya viwanda mbalimbali.
“Umeme kukati kati pamoja na wakati mwingine kuwa mdogo kabisa ni moja ya vikwanzo vinavyosababisha kusitisha uzalishaji wakati mwingine kwa kuhofia kuungua kwa mashine hali inayosababisha hasara kubwa kwa
kiwanda”alisema Tamimu
"Kwa Mkoa wa Tanga waone umuhimu wa kupunguza au kumaliza tatizo la
hitilafu ya umeme,kwani haitakuwa na maana, Mkoa una viwanda vya
Saruji Vingi halafu bei ni sawasawa na maeneo ambayo hakuna kiwanda,"
alisema Mkurugenzi huyo
Akiongela kuhusu miundombinu ya reli alisema iwapo itaimarishwa
kote nchini itaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa gharama za
usafirishaji wa bidhaa zao wanazizalisha kwenda kwenye masoko.
"Ili maendeleo yawepo katika sekta ya viwanda ni lazima reli ifanye
Kazi kwani itasaidia kupunguza gharama, kwani kwa sasa gharama kubwa
ipo kwenye usafirishaji wa bidhaa" alisema Tamimu.
Hata hivyo Mkurungenzi huyo aliwashauri wazalishaji wa hapa nchini
kuhakikisha wanakuwa na malengo ya kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitaweza kuuzika kwa urahisi hata nje ya nchi.
Tamimu alisemanini ni lazima uzalishaji wetu ulenge kuuza katika
masoko ya kidunia baada ya kutegemea masoko ya ndani kwani hapo ndio
tutaona faida ya sekta hiyo.
"Kama bidhaa kutoka nje zinauzika mpaka huku kwetu kwani ni nasie
tusiwe na malengo ya kushika hayo masoko ya kwao ili nchi yetu iweze
kufaidika na fursa hiyo" alisisitiza Mkurugenzi huyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni