Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na
Mawasiliano Prof Makame Mbarawa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Maritini
Shegella kusimamia ulipaji we fidia kwa watakaopisha Mradi wa bomba la Mafuta
litakalo jengwa kutoka Mkoani Tanga kwenda nchini Uganda.
Waziri Mbarawa ameyasema hayo wakati
akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na maofisa wa Bandari ya Tanga
wakati wa ziara yake mwishoni wa wiki mkoani hapa na kupewa taarifa juu ya
Mradi wa bomba la Mafuta kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Maritini Shegella.
Amesema mradi huo ni Wawatanzania
wote na sio watu wachache ambao watataka kuuhujumu na kujinufaisha wenyewe.
Aidha Mkuu wa Mkoa Maritini Shegella
amemuomba Waziri kuwasaidia upatikanaji wa vifaa katika Bandari ya Tanga kwani
inachangamoto ya Wateja huchukuwa muda mrefu hivyo kuchelewesha maendeleo. Make
Money Online :
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni