Daraja la Lumesule likiwa katika hatua ya ujenzi katika barabara ya Mangaka – Lumesule – Nakapanya (70.5km)
Wakala wa Barabra Tanzania (TANROADS) yenye jukumu
la kuratibu na kusimamia matengenezo, ukarabati na ujenzi wa barabara kwenye
mtandao wenye urefu wa jumla ya kilometa 34,333. Kati ya hizo
kilomita 12,203 ni barabara kuu na kilomita 22,130 ni barabara za mkoa.
Pia kuboreshwa kwa hali ya
usafirishaji kutaanza na kuchochea shughuli za kijamii na kiuchumi kati ya
mikoa ya Lindi na Mtwara na nchi ya Msumbiji na pia nchi za ukanda wote wa
Maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor).
TANROADS imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika
ujenzi wa barabara na madaraja nchini kote, Tukimulika ukanda wa kusini wa
Tanzania yaani Mtwara – Masasi – Tunduru – Songea – Mbamba Bay (km 860
hadi Lilongwe nchini Malawi km 1263), barabara hupitika vizuri na sehemu chache
ambazo ziko katika hatua za awali za ujenzi hupitika kwa taabu wakati wa
masika.
Miradi mikubwa ya barabara na madaraja inayoendelea
kutekelezwa ukanda wa maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor) ni
Mangaka – Lumsule – Nakapanya (70.5km), Tunduru – Matemanga (58.7 km) na
Kilimasera – Namtumbo (60.7 km).
Barabara hizi zilizo katika hatua nzuri ya
utekelezaji wa ujenzi ni muhimu kwenye ukanda wa maendeleo wa kusini na
inatarajia kuwa barabara ya kimataifa (international route) itakayounganisha
nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na Msumbiji kupitia daraja la Umoja (Unity
Bridge) punde ujenzi unaendelea wa barabara ya Mangaka – Mtambaswala (65.5 km)
utakapo kamilika.
Dhumuni kubwa la miradi hii ni kuendeleza sehemu ya
kusini yenye utajiri wa mazao ya kilimo, madini na utalii ambazo ni muhimu kwa
maendeleo. Kama ilivyo kwa mikoa ya kusini zao kuu katika eneo la mradi ni
korosho.
Ujenzi wa Barabara ya ukanda huu kwa kiwango
cha lami utakapokamilika muda wa safari utapungua, idadi ya magari yanayotumia
barabara itaongezeka na usalama wa watumiaji wa barabara utaboreka na hivyo
gharama za usafiri na usafirishaji zitapungua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni