Alhamisi, 29 Septemba 2016

UTAFITI WA TWAWEZA UMEBAINI ASILIMIA 80 YA WANANCHI WANATAKA MAENDELEO NA SI SIASA.

ASILIMIA 80 ya Watanzania wamesema juhudi za maendeleo hazina budi kupewa kipaumbele baada ya uchaguzi na kukataa mikutano ya kisiasa ambayo wanadai hukwamisha shughuli za  maendeleo.

Taarifa ya utafiti huo iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaaam na Shirika la Utafiti la TWAWEZA ilisema kuwa utafiti huo umebeba maoni ya wananchi kuhusu  demokrasia, udikteta na maandamano nchini Tanzania.

Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa takwimu za muhtasari huo  zinatokana na na utafiti wa sauti za wananchi ikiwa ni moja ya programu za Twaweza.

Pia katika utafiti huo, wataalamu hao waliweza kubaini kuwa asilimia 49 ya wananchi wanakubaliana na kuzuiwa kwa mikutano ya vyama vya siasa kutokana na kwamba huvuruga umakini wa Serikali na Wananchi.

Katika suala la kumhusisha Rais Maguli na udikteta utafiti huo umebaini kuwa asilimia 58 ya Watanzania wanapinga uwepo wa udikteta katika serikali ya awamu ya Tano ya Rais John Magufuli.

Aidha utafiti huo wa Twaweza pia umebainisha kuwa asilimia 50 ya wananchi wamesema hakuna uwezekano wa wao kushiriki kwenye maandamano yoyote.

Kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kuzuia mikutano ya hadhara utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 60 wanamuunga mkono Rais katika kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa.

Utafiti huo wa Twaweza umekuja baada ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kujipatia pongezi nyingi kwa jitihada zake za kupambana na na vitendo vya rushwa.

SERIKALI YA TANZANIA YARIDHIA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA .

SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. 
 
Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika  tarehe 29 Septemba, 2016  Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. 
 
Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020. 
 
Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania. 
 
Mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda. 
 
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku ambapo kila pipa litaliingizia taifa Dola za Marekani 12.2. 
 
Amebainisha kuwa pamoja na kusafirisha mafuta ya kutoka nchini Uganda bomba hilo pia linatarajiwa kusafirisha mafutakutoka nchi nyingine zaJ amhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudani Kusini ambazo zimeonesha nia ya  kusafirisha mafuta yao kupitia bandari ya Tanga. 
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja faida nyingine ambazo Tanzania itazipata kutoka na namradi huo kuwa ni kupatika na kwa ajira zaidi ya 15,000 wakati wa ujenzi na ajira 2,000 baadaya ujenzi kukamilika, kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia, kukuza biashara katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, kampuni za ujenziza Tanzania kupata kazi za ujenzi. 
 
Aidha, amesema Tanzania inatarajia kunufaika zaidi kwa kutumia bomba hilo kupitisha mafuta yanayotarajiwa kupatikana katika maeneo ya ziwa Tanganyika na Ziwa Eyasi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, SEPTEMBA  28, 2016 

SERIKALI YATENGA BIL 100 KUKARABATI VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA.

irin


SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Magufuli imetenga kiasi cha sh. Bil. 100 katika bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa viwanja mbalimbali vya ndege nchini.

Rais Dk. Magufuli alisema hayo juzi katika sherehe za uzinduzi wa ndege mbili za Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na serikali, kwenye Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo viwanja hivyo vitaboreshwa ili kuwezesha ndege hizo kutua bila wasiwasi.

Mhe. Rais akifafanua zaidi, alisema , kiwanja cha ndege cha Nduli kilichopo umbali wa kilometa 13 Kaskazini Mashariki mwa Manispaa ya Iringa, ambacho kipo kwenye kiwango cha lami kitakarabatiwa, ili ndege hizo zitue na kupaa bila tatizo.

Dk. Magufuli alisema, kiwanja cha Nduli Iringa ni kiunganishi kikubwa na JNIA na kitatumika kupeleka watalii wanaokwenda kutembelea mbuga ya wanyama ya Ruaha, wakitokea Mataifa mbalimbali duniani.

Alisema mbali na kiwanja hicho cha Nduli, pia kiwanja cha Musoma kitawekwa lami, ili nacho kiwe moja ya maeneo ndege hiyo itakwenda, na kurahisisha usafiri wa watalii watakaokwenda kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti. Kwa sasa kiwanja cha Musoma kipo katika kiwango cha changarawe na kinatumika kwa ndege mbalimbali kutua na kupaa.

Kwa mujibu wa Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Nduli, Bi. Hannah Kibopile, kiwanja hicho kinapokea ndege ndogo zaidi ya saba zenye uwezo wa kubeba abiria 13, na kati ya hizo tatu zipo kwenye ratiba maalum ya kila siku na zilizosalia ni za kukodishwa na nyingine zinakwenda mbuga ya wanyama ya Ruaha.

Bi. Kibopile alisema ndege zinazotua kwenye kiwanja hicho zinatoka Jijini Dar es Salaam, Sumbawanga, Songea na Mbuga ya Ruaha.
Naye Kaimu Meneja wa Musoma, Bi. Faraja Mayugwa amesema kiwanja hicho kinapokea ndege zaidi ya nne kwa siku na nyingi zinakuwa za kukodi zinazopeleka watalii mbugani.

Katika hotuba yake, Rais Magufuli alisema “Hii ndege inaweza kutua katika kiwanja cha aina yeyote; na serikali itaendelea na ukarabati wa viwanja vya ndege vya pembezoni, ili viwe katika kiwango, ambacho ndege hizi zitatua na kuruka bila wasiwasi,”.

Akifafanua zaidi Dk. Magufuli alisema serikali inatarajia kununua ndege nyingine kubwa mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 160 na 242, ambazo zitaanzia safari zake kwenye JNIA kwenda sehemu mbalimbali duniani kama China au Marekani moja kwa moja, ikiwa ni lengo la kupata abiria hao, ambao wengi wao watakuwa watalii wanaokuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali. Bombardier inauwezo wa kubeba abiria 76.

Naye Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof Makame Mbarawa awali wakati akimkaribisha Mhe. Rais kuzungumza na wananchi katika ghafla hiyo ya uzinduzi wa ndege, alisema kwa kuanzia ndege hizo zitatua kwenye viwanja 11 vya ndege, ambavyo ni Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro (KIA), Zanzibar (AAKIA), Mwanza, Dodoma, Arusha, Bukoba, Kigoma, Tabora, Mbeya na  Mtwara.  Pia ndege hiyo itakwenda Comoro.

Mhe. Prof. Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuendelea kufanya upembuzi yakinifu kwa kuangalia viwanja  vingine vya ndege, ambavyo ndege hizi zitakwenda.

MAMLAKA YA MAJISAFI JIJINI TANGA (TANGA UWASA) YAKUTANA NA WADAU.


Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Milapwa akizungumza na wafanyakazi pamoja na wadau wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Tanga Uwasa)
Meneja wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mzingira jijini Tanga (Tanga Uwasa) akizungumza na wadau wa Mamlaka hiyo kwenye kikao cha pamoja.


Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga Uwasa Haika Ndalama akitoa ufafanuzi wa jambo kwenye kikao na wadau.

 Afisa Mahusiano wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dora Killo akitoa elimu katika mkutano walio uandaa.



TANGA.
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Tanga Uwasa) jijini Tanga imetakiwa kujipanga ili kuhakikisha inaboresha huduma ya sekta ya majisafi na majitaka mjini Tanga.

Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Milapwa katika ufunguzi wa mkutano wa wafanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na wadau wa maji pamoja na madiwani wa wilaya ya Tanga katika ukumbi wa Veta mkoani hapa.

Milapwa alisema Mamlaka ya maji safi ijipange kutoa haki kwa wateja wake na kusikiliza ushauri wa wadau wa maji kwa kufanya hivyo itakuwa imeondoa mapungufu na kuboresha huduma kwa wahitaji wake.

Naye Meneja wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira (Tanga Uwasa) jijini Tanga Mohamed Pima alisema wamejipanga kuhakisha huduma ya maji safi na salama yanatosheleza kwa wakazi wa jiji la Tanga na pembezoni mwa jiji hili kwa asilimia 96.9.

Pima alisema Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira jiji la Tanga inatoa huduma ya kuunganisha maji ndani ya siku saba tu na sio zaidi kwa wale wateja wapya kwa huduma bora na yaharaka ni Tanga Uwasa.

Pia Katibu Tawala mkoa wa Tanga Zena Said na mjumbe wa bodi ya Tanga Uwasa aliiomba Tanga uwasa kuwasaidia wateja kwa kuwapatia mafundi bora wa kujenga mashimo ya kuhifadhia maji taka ili kuepuka ujenzi olela na usio na ubora.

Zena alisema majitaka ni tatizo na ujenzi wa mashimo yasiyo na kiwango yanayosababisha kuvuja na kusambaa kwa maji taka mitahani na kuwanyima raha wateja.

Aliutaka uongozi kuwasaidia wananchi kupata mafundi wenye ubora wa kujenga miundo mbinu ya maji taka katika nyumba zao.

Kwa upande wake Meya wa jiji la Tanga na Diwani wa Nguvumali Selebose Mustapha aliuomba uongozi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kujitahidi kuweka vituo vya kutolea malalamiko katika maeneo ya karibu na wananchi kwani kwa sasa jiji linakuwa na uhitaji wa huduma  majisafi ni mkubwa .

Selebose aliwataka wafanyakazi wa Tanga Uwasa kupitia mitaani mara kwa mara katika maeneo korofi ya mabomba ya maji taka ili kukabiliana nazo na kufanya kuendelea kuwa mamlaka bora kwa kutoa huduma maeneo yote na kuondoa  kero za wananchi.

Kaimu mkurugenzi  mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na Uasfi wa mazingira(Tanga Uwasa) Haika Ndalama alisema kero zote zilizotolewa na ushauri wote wao kama Mamlaka watazichukuwa na kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo.

Ndalama alisema ili Mamlaka iweze kufanikiwa kujiendesha wateja wanatakiwa walipe bili kwa wakati na kupitia Bank ya CRDB au NMB au M-pesa na Tigo pesa kwani kwasasa Mamlaka haipokei pesa tasilm. 
 
Alisema wafanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira wamejipanga kutoa huduma kwa kushirikiana na wananchi ili kuwafikia wote kwa huduma iliyo bora zaidi.