Jumatano, 31 Agosti 2016

TAARIFA TOKA IKULU: RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Agosti, 2016 amemteua Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).

Bw. Doto M. James ataapishwa kesho tarehe 01 Septemba,2016 saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
                                                        31 Agosti, 2016

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni