Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ufunguzi wa mkutano wa majadiliano
kuhusu uboreshwaji wa utekelezaji wa matakwa ya viwango uliofanyika hapo jana
Jijini Tanga.
Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia
kuweka mazingira mazuri ya kiutendaji yasiyo na muingiliano au mgongano wa
kimaslahi ikiwemo kulinda mazingira na kuiepusha jamii na athari za kiafya
zitokanazo na utumijai wa bidhaa zisizo na viwango.
“Natambua juhudi kubwa ambazo
zimekuwa zikichukuliwa na taasisi kama TBS,TFDA na nyingine nyingi katika swala
la udhibiti wa bidhaa hafifu lakini ifike wakati muweze kushirikiana ili kuweza
kupata matokeo bora “alisema RC Shigella.
Hata hivyo alizishauri taasisi hizo
kuona umuhimu wa kushirikisha taasisi binafsi katika mipango yao ikiwemo
wazalishaji wa bidhaa pamoja na waagiza ili waweze kuwa na uelewa mpana wa
kudhibiti uwepo wa bidhaa duni hapa nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurungenzi
mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania TBS Kezia Mbwambo alisema kuwa kutoka na
changamoto ya uingiaji wa bidhaa duni katika hususani mikoa iliyoko kando kando
ya bahari ya hindi ndio imewalazimu kuitisha kikoa hicho kuona namna bora ya
kujadiliana na kufikia mwafaka.
Alisema kuwa mikoa ya pwani ndio
njia kuu ya kuingilia bidhaa ambazo hazina ubiora na wakati mwingine hata
bidhaa ambazo zinazalishwa nchini zilizochini ya viwango inakuwa rahisi
kusafirishwa.
“Tunakutanisha wadau ili tuweze
kujadili kwa pamoja kwa kutumia fursa zilizopo kwa kufanyakazi pamoja na
ilikuweza kupunguza raslimali zilizopo na kuweza kushirikina na katika ukaguzi
na udhibiti wa bidhaa duni”alisema Mbwambo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni