Jumatano, 10 Agosti 2016

SERIKALI IMEJIPANGA KUONDOA MSONGAMANO KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.



Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizinduwa safari za gari moshi jana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita wakiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipanda katika gari moshi ambalo safari zake zimezinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakiwa katika usafiri wa gari moshi uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
Safari ikiwa inaendelea katika mabehewa na baadhi ya watendaji wa TRL gari moshi kati ya Pugu jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

HABARI KAMILI
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanakuwa na usafiri wa uhakika katika kuondoa msongamano wa magari mjini kwa kutumia usafiri wa gari moshi.

Hayo ameyasema na Profesa Mbarawa wakati wa uzinduzi wa gari moshi linalofanya safari zake kuanzia Stesheni hadi Pugu, amessema kuwa kuanza kwa usafiri huo umepunguza daladala 45.

Profesa Mbarawa amesema katika hatua nyingine wanaangalia usafiri kwa njia ya boti katika baadhi ya maeneo na wataalam walishafanya kazi hiyo.

Aidha amewataka wafanya kazi kuacha kufanya kazi kwa mazoea kama walivyokuwa wakifanya na watakaofanya hivyo hawatavumiliwa ikiwa ni pamoja na kufisadi mali za reli.

Hata hivyo amesema waliojenga katika miundombinu ya reli wanatakiwa kubomolewa kwani kuwepo kwa nyumba hizo katika miundombinu hiyo ni kosa kisheria.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wakazi wa Dar es Salaam wataondokana na foleni kutokana na jitihada mbalimbali.
Amesema moja jitihada hizo ni kuondoa malori ya mafuta ambapo mafuta yatasafirishwa kwa njia ya bomba mpaka Chalinze na kuanza kwa safari ya mikoani.

Meya wa Jiji, Isaya Mwita amewataka wananchi kutumia usafiri huo kutokana na kutokwa na foleni na gharama yake kuwa nafuu.

Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema usafiri umeanza kutokana na nguvu ya serikali karibu katika utoaji wa huduma ya usafiri huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni