Mwanasheria Mkuu wa Serikali George
Masaju aonya vyama vya siasa kutumia maneno yanayovunja amani na usalama wa
nchi.
Masaju ambaye amezungumza na
wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo, ametolea mfano
Oparesheni UKUTA iliyotangazwa kufanywa na CHADEMA na kusema kuwa ina maneno ya
kijeshi yanayotumiwa kwenye shughuli za kihalifu.
Amesema neno UDIKTETA siyo sahihi
kwa kuwa nchini Tanzania hakuna udikteta kwa kuwa serikali inafanya shughuli
zake kwa mujibu wa sheria na nchi inaendeshwa kwa kuzingatia mgawanyo wa
madaraka wa katika miimili yote mitatu ya dola.
“UKUTA lengo lake ni nini, sawa
na kuwatenganisha wananchi na serikali yao” Amesema Masaju na kuwataka wananchi
kutambua kuwa Septemba Mosi ni siku ya Majeshi nchini huku akishangazwa na
CHADEMA kuchagua siku hiyo kuzindua kampeni yao aliyodai kuwa ina lengo la
kuvuruga nchi.
Masaju amewataka viongozi wa vyama
vya siasa nchini kutii mamlaka za dola ikiwemo Jeshi la Polisi na mahakama
iliyowapa mwongozo juu ya ombi la kupinga zuio la jeshi la polisi na pia
kufuata ushauri waliopewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora juu ya
kutokuwepo kwa udikteta nchini.
Amesema sababu kuu za kuzuia
Oparesheni ni mbili ambazo ni hali ya usalama kutokuwa shwari, pamoja na
kutokuwepo kwa udikteta nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni