Mbunge wa Jimbo la Tanga
(CUF) Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO)
Dkt Asha Mahita
Wadau kutoka mbalimbali wakimsikiliza Mbunge wa Tanga Mussa Mbaruku katika mzungumzo na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita.
MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CUF), Mussa Mbaruku ameombwa kuangalia namna ya kuweka
mkakati wa kuvisaidia vituo vya afya na Zahanati zilivyopo ndani ya Jiji la
Tanga ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya mkoa wa Tanga
Bombo inayohudumia wagonjwa wa mkoa mzima.
Ombi
hilo lilitolewa na Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO) Asha Mahita wakati
Mbunge alipotembelea hospitali na kuona msongamano unaoikabili
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa unatokana na kutokuwepo na ubora katika zahanati na
vituo vya afya jambo ambalo linalowafanya wanachi kukimbilia katika Hosptiali
hiyo.
Pia alisema iwapo kutakuwa na mabororesho katika vituo hivyo huku Serikali na wadau
mbalimbali wakiweka nguvu zao katika swala la kumalizia Hospitali ya wilaya
ambayo mpaka sasa inajengo moja la ghorofa kwa ajili ya utawala ikimaliziwa na
kuanza kutumika kutapunguza kwa asilimia kubwa msongamano kwenye hospitali
hiyo.
Kwa
upande wake, Mbunge Mussa Mbaruku alihaidia kuangalia namna ya kuzipatia
ufumbuzi changamoto hizo kwani wananchi afya zao zinapokuwa zimeimarika
inawasaidia kuweza kufanya shughuli za kujenga taifa na kujiingizia kipato.
“Ndugu
zangu huu si muda wa kupiga porojo kuhusiana na masuala ya afya ambalo ndio uti
wa mgongo wa wananchi hivyo lazima viongozi wajenge umoja na kutafuta
njia ya kuweza kuviboresha vituo hivyo ambavyo vitawasaidia kwa asilimia kubwa
wananchi kupata huduma hiyo kwa ukaribu zaidi “Alisema Mbunge Mbaruku.
Aidha
alisema pamoja na changamoto zinazozikabili zahanati na vituo hivyo lazima
Serikali itenge fedha za kutosha ili kuweza kuimalizia Hospitali ya Wilaya
iliyopo Masiwani Shamba ambayo mpaka sasa bado hakuna majibu sahihi ya kukwama
kwa umaliziwaji wa Hosptili hiyo.
“Bado
nashindwa kupata majibu ni kitu gani kinachokwamisha kumalizika kwa Hospitali ya
Wilaya ambayo tayari inajengo zuri la utawala tena la ghorofa serikali
inawajibu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Hospitali hiyo
inamalizika na inakuwa na kiwango bora katika sekta zote za matibabu.
Mbaruku
alifanya mazungumzo hayo na mganga mkuu wa Mkoa alipo watembelea madaktari kutoka
katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim Volunteer huku
wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza, Afrika kusini,
Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa ajili ya kutoa
matibabu bure ya Fistula.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni