Ijumaa, 12 Agosti 2016

MADAKTARI BINGWA KUTOKA NCHI YA UJERUMANI WAFANIKIWA KUOKOA MGUU WA KIJANA KWA KUMFANYIA UPASUAJI ULIOCHUKUA MASAA 10.



 Madaktari bingwa kutoka Ujerumani wakifanya kazi ya kurekebisha mguu wa kijana aliyekuwa hatarini kukatwa mguu katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo mkoani Tanga
 Mguu wa kijana aliyekuwa amelazwa kwa muda mrefu katika hospitali ya Bombo Tanga ukiwa umerudi katika hali yake.

HABARI KAMILI.
 MADAKTARI Bingwa kutoka nchini Ujerumani wakiongozwa na Dr. Rudiger Herr wameweza kuwasaidia watanzania 46 waliokuwa na matatizo mbalimbli ya kurekebisha maumbile pamoja na midomo sungura (plastic surgery) katika Hospital ya Rufaa ya Bombo mkoani Tanga.

Akizungumza wakati anatoa taarifa ya Upasuaji uliofanyika kwa madaktari wa Hospitari ya Rufaa ya Bombo Prof. Jugen Dolderer “amesema wemeweza kufanikiwa kufanya upasuaji ambao yawezekana haujawai tokea katika nchi ya Tanzania kurekebisha kidonda kikubwa kilichokuwa mguuni kwa kijana mwenye umri wa miaka 20 ambae mguu wake ulikuwa hatarini kukatwa kutokana na kidonda alicho kuwa nacho na sasa anaendelea na matibabu ”

Prof. Jugen Dolderer amesema upasuaji wa kijana huu ulichukua masaa 10 hali ambayo kwa kukata nyama na kimfupa na mishipa kutoka begani na kushona katika eneo lenye kidonda.

Pia Mratibu wa zoezi la Upasuaji wa Kurekebisha Maumbile (plastic surgery) Dkt Waless Karata wa Hospital ya Rufaa Bombo amesema watanzania wanatakiwa kujitoa kwa hali na mali kuwasaidi Madaktari hawa Mabingwa wanao jitoa kwajili ya watanzani wenye uhitaji.

Amesema wamefanikiwa sana kwa upasuaji mkubwa walioweza kuufanya kwa watu 46 ambao sasa wanaendelea vizuri na matibabu.

“Wajerumani hawa wamekuwa msaada mkubwa na wanafanya kazi kubwa kwa muda wa wiki mbili tu tangu waingie katika Hospitali ya Bombo wamekuwa wakifanya upasuaji na kuwapa faraja wagonjwa wanao wafanyia upasuaji kwa kazi hizi Madaktari wa Tanzania tunatakiwa kuiga mfano wao amesema Dkt Karata”

Nao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi ambao wengine walipata ajali ya moto wameiomba Serikali  kutoa kibali kwa Madaktari hawa Mabingwa kuja nchini ili kuwasaidia watu wasio na uwezo kwani upasuaji huu unahitaji gharama kubwa katika mahospital lakini wao wamepata huduma hii bule walisema wakati wakiwashukuru Madaktari.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni