Jumatatu, 29 Agosti 2016

MWIGURU NCHEMBA ALETA KIAMA KWA WAINGIZA MADAWA YA KULEVYA NCHI.


Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Tanga.

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akizungumza na Askari Mkoani Tanga.

HABARI KAMILI.
 


Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya siku moja katika mkoa Tanga kuangalia hali ya ulinzi na usalama wa mkoani humo.

Akizungumza na askari wa ulinzi na usalama waziri amewataka kupambana na waalifu wa magendo na madawa ya kulevya yanayopitishwa kwenye vichochoro na bandari bubu zilizopo mkoani Tanga.

“Ninajua juhudi mazozifanya askari  lakini nahitaji muongeze juhudi zaidi kupambana na magendo yanayopita katika bandari bubu na vichochoro ndani ya mkoa huu” alisema waziri.

Waziri pia aliwataka askari kupambana na waingizaji wa madawa ya kulevya wanaopitisha katika mipaka ya mkoa huu na kuwakamata wale wote wanao uza madawa hayo rejareja yanayo athili nguvu kazi ya Taifa wakamatwe. 

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii kuacha kufanya vitendo vinavyoleta uvunjifu wa amani wa nchi yetu.

Pia amewataka askari kuwalinda raia na mali zao na  kuwakamata wale wote wanao hamasisha uvunjifu wa amani kwani kulinda amani ni jukumu la kila mmoja wetu.

Waziri Mwigulu amewaonya wale wote wanaofanya biashari ya kupitisha wahamiaji haramu kwa njia zisizo rasmi biashara hiyo waache mara moja maana mkono wa sheria utawafikia.

Waziri amemalizia kusema Usalama wa raia si mjadala wala si jambo la hiyari wote tutii sheria za nchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni