MKUU WA MKOA WA TANGA NA VIONGOZI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI WAKITEMBELEA ENEO MAALUMU LA UJENZI WA MATANKI YA MAFUTA
MKURUGENZI WA JIJI LA TANGA DAUDI MAYEJE AKIJIBU MASWALI YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU FIDIA YA WALIOKUWA WANAMILIKI ENEO HILO. |
MKUU WA MKOA WA TANGA MARTIN SHIGELLA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWENYE ENEO HILO |
KAIMU MENEJA WA MAMLAKA YA BANDARI YA TANGA HENRY ARIKA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAANDALIZI YA MRADI HUO. |
KAIMU KAMISHINA MSAIDIZI WA PETROLI WIZARA YA NISHATI NA MADINI MWANAMANI KIDAYA WA PILI KUTOKA KUSHOTO AKIELEZA KURIZIKA NA MAANDALIZI YA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA.
MWANASHERIA WA PETROLI NGABO IBRAHIMU AKIWASHUKURU UONGOZI WA MKOA WA TANGA.
MKUU WA MKOA WA TANGA MARTIN SHIGELLA AKIJARIBU KUENDESHA GREDA LINALOSAFISHA ENEO LA MRADI HUO. |
HABARI KAMILI
Wizara ya nishati na madini
imeridhishwa na jitihada za viongozi wa mkoa wa Tanga katika maandalizi ya
kupokea mradi mkubwa wa bomba la mafuta linao
jumuisha nchi mbili ya uganda na Tanzinia.
Akizungumza kwenye eneo
maalum ambalo limeandaliwa kwa kujengwa matanki makubwa ya kupokea mafuta katika kijiji cha chongeleani mkoani Tanga Kaimu kamishna msaidizi wa Petroli
wa Wizara ya Nishati na Madini Mwanamani Kidaya amesema amelizika na maandalizi
ya awali kupokea mradi huo mkubwa katika ukanda wa jumuiya ya afrika mashariki.
Naye mkuu wa mkoa wa Tanga
Martin Shigela amesema wananchi mkoani Tanga wamejianda vizuri kupokea mradi
na mkoa kwa ujumla Umejipanga kuwashuhulikia wale wote wenye nia mbaya ya
kukwamisha mradi wenye manufaa kwa mkoa na taifa kwa ujumla.
“Hatuta kuwa tayari
kumfumbia macho yeyote Yule mwenye ana nia ya kuvuruga mradi huu iwe ni
mwanasiasa au mtu yeyote tutamshuhurikia” alisema Shigela.
Hata hivyo kaimu meneja wa
bandari Herny Arika amesema wamejipanga kwaajili
ya upokeaji wa mizigo itakayo kuja Bandari kwaajili ya ujenzi wa bomba la
mafuta na mpaka sasa mkakati inaendelea vizuri.
Pia bandari imetenga kiasi
cha Bilion 9.2 kwa ajili ya kuongeza gati na kuimarisha ulinzi kwa kutumia
vifaa vya kisasa na kuongeza kujenga eneo la kuhifadhia mizigo amesema Arika.
Kwa upande wake mkurugenzi
wa Jiji la Tanga Daudi Mayeje amesema Halmashaul ya Jiji la Tanga inawaomba
wananchi wawe watulivu na serikali itawalipa wahusika wote wa eneo husika fidia
zao na waache kusikiliza maneno yasiyo na manufaa kwao.
Mayeje amewahimiza wakazi
wa mkoa wa Tanga kutumia fulsa za kibiashara zitakazo jitokeza endapo ujenzi wa
miundombinu ya bomba hilo kutengama ili kujikwamua kiuchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni