Kamanda wa polisi
Leonard Poul akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jinsi walivyo uwawa watu
wawili wanaoshukiwa ni majambazi jijini Tanga.
Kamanda wa polisi
Mkoani Tanga, Leonard Poul, akiwaonyesha waandishi wa habari dawa ambayo vibaka
wamekuwa wakiitumia kupuliza katika madirisha ya nyumba usiku na kwenye vioo
vya magari na ambavyo hulainisha na kuweza kuiba kwa urahisi.
Kamanda wa polisi Mkoani
Tanga, Leonard Poul, akiwaonyesha waandishi wa habari kioo cha gari
kilichopakwa dawa na kulainika na wizi kufungua mlango na kuiba vitu
vilivyokuwemo ndani.HABARI KAMILI;
JESHI la Polisi Mkoani hapa
limewauwa watu wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi kwa kuwapiga
risasi wakati wa majibizano ya risasi
kwenye msitu wa Pongwe nje kidogo ya jiji la Tanga.
Majambazi hao ambayo kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Tanga,
Leonard Poul, amesema kwa wiki mmoja mfululizo walikuwa wakifanya uporaji
kwenye maduka makubwa na kumpora Raia mmojawa kigeni.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake, kamanda Poul
amesema utupianaji wa risasi ulianzia mjini Tanga baada ya majambazi hao kukimbia baada ya
kufanya uporaji.
Kamanda amewapongeza waendesha pikipiki maarufu kama
Bodaboda kwa ushirikiano wao kwa kushiriki kikamilifu kuwafukuza majambazi hao
hadi kwenye msitu wa Pongwe na kufanikiwa kuwauwa.
Amesema kuuwawa kwa majambazi hao kulitokana na kuishiwa kwa
risasi walizokuwa na nazo na badala yake kujificha kwa kupanda katika miti na
wakati wa msako huo walionekana wakiparamia juu ya miti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni