Jumatano, 24 Agosti 2016

WATOTO WAPEWE HAKI ZAO WANYONYESHWE SIKU ELFU MOJA ZA AWALI.

Utafiti unaonyesha wamama wengi awazingatii unyonyeshaji wa watoto  ili kuendelea kupambana na tatizo la udumavu kwa watoto hapa nchini, wakina mama wajawazito wanatakiwa kuzingati unyonyeshaji wa siku elfu moja za awali.

Akitolea ufafanuzi swala hili Daktari wa kituo cha afya Makole mkoani Dodoma Dkt Sauda Mutabazi amesema kwa wanawake wanatakiwa  kuzingatia unyonyeshaji sahihi kwa mtoto kwani kutasaidia uboreshaji wa afya ya mtoto na hata kusaidia kuwa na maendeleo mazuri awapo shuleni.

Akielezea umuhimu wa utumiaji wa vidonge vya madini chuma kwa mama mjamzito Dkt Sauda amesema vidonge hivyo viliweza kumsaidia yeye akiwa mjamzito na faida aliyoipata kwa kutumia vidonge hivyo wakati akiwa mjamzito.

“nilishiliki kutumia vidonge vya madini chuma na vidonge vya kuongeza damu  pindi nilipokuwa mjamzito vinasaidia kuzuia matatizo madogodogo na kumkinga mtoto na kuniongezea damu kipindi chote cha mimba.

Pia Dkt Sauda alisema muda sahihi wa utumiaji wa vidonge vya madini chuma kwa mama mjamzito ili asipatwe na shida ya kichefuchefu kama ambavyo wengine hupatwa mara baada ya kutumia vidonge hivyo.

“Ni vizuri Mama mjamzito  ameze dawa hizi wakati akiwa amepata chakula kizito na  muda mzuri ni wa usiku wakati unataka kulala “alisema Dkt Sauda.

Inaaminika kuwa ili mtoto aweze kuwa na maendeleo mazuri na afya bora ni vema wazazi kushirikiana kwa pamoja katika kumnyonyesha mtoto kwa siku elfu moja za awali.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni