MIUNDO MBINU YA BARABARA ILIYOPO NCHINI TANZANIA
BOMBA LA MAFUTA LA TAZAMA LA KUTOKA TANZANIA KWENDA ZAMBIA .
FAHAMU SABABU 9 ZILIZOWAVUTIA WA UGANDA KUICHAGUA BANDARI YA TANGA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI.
Kwanza, bandari ya Tanga ni bora kwa sababu ina kina kirefu kulinganisha na bandari za mombasa na Lamu. Bandari ya Tanga ina kina cha zaidi ya mita 23 ambayo kimataifa inatakiwa ili meli kubwa inayokuja kuchukua shehena ya mafuta iweze kutia nanga na kupakia mafuta nakuondoka, tumewapiku wenzetu kwa kina ambapo bandari ya Lamu ina kina cha urefu wa mita 18.
Pili, bandari ya Tanga inaweza kufanya kazi kwa siku zote za mwaka Hii ni tofauti na bandari za Kenya ambazo zinaathiriwa na pepo mbalimbali zinazovuma kwa majira tofauti ya mwaka hivyo kuathiri utendaji kazi.Tatu ni Miundombinu iliyopoa Tanzania ambapo tayari inarahisisha usafirishaji wa vitendea kazi na pia usafiri wa watu kwenda maeneo mbalimbali ambapo bomba hili litajengwa, Reli ya Tanzania inatarajiwa kusafirisha mabomba 123,000 pindi ujenzi utakapoanza, Hii ni tofauti na Kenya ambapo wao miundombinu ni changamato hivyo ingewalazimu wao kujenga kwanza barabara ndipo waweze kujenga bomba la mafuta.
Nne ni kuwa bandari ya Tanga tofauti na bandari ya Lamu itazipa nchi nyingine zilizopo ukanda wa Africa Mashariki urahisi wa kutumia bomba hilo, Nchi hizo ni kama Kenya, Sudan Kusini, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Tano ni uzoefu wa Tanzania miradi ya ujenzi wa maboma yenye urefu mkubwa, Tanzania imeshajenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Slaam lenye urefu wa kilomita 542, Lakini pia Tanzania imejenga bomba la mafuta la Tanzania Zambia Mafuta (TAZAMA) lenye urefu wa kilomita 1705 linaloanzia Dar es Salaam Tanzania hadi Ndola Zambia.
Sita ni kuwa Uganda ilichagua bandari ya Tanga kwani maeneo yote bomba hili litakapopita hakuna makazi makubwa ya watu hivyo fedha kwa ajili ya fidia hazitakuwa kubwa kama bomba hili lingepita Kenya kwenda bandari ya Lamu.
Saba, maeneo yote ambapo bomba hili litapita kutokea Uganda hadi kufika bandari ya Tanga ni maeneo tambarare na halipiti katika hifadhi ya mbuga za wanyama.
Namba nane ni suala la gharama, Serikali ya Kenya ingeitoza Uganda shilingi 1,280 kwa kila pipa ambalo ingelipitisha katika ardhi yake, ila kwa upande wa Tanzania haitawatoza Uganda fedha kwa kila pila pipa wakipitisha mafuta hivyo kufanya unafuu kwa Uganda.
Tisa ni suala la ulinzi, Uganda iliamua kupitisha bomba lake la mafuta Tanzania kutokana na masuala ya kiusalama ambapo kuna hatari kubwa sana kwenye usalama wa mafuta hayo kama yangepitishwa nchini kenya ambapo kumekuwa na mashambulio mbalimbali ya kigaidi yalitotekelezwa na kundi la Al- Shabab.
Bomba hilo litaingilia Mkoa wa Kagera kutoka nchini Uganda na kupita katika mikoa ya Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi Bandari ya Tanga. Bomba hilo linatarajiwa kukamilika mwaka 2020 katikati.
KARIBU BOMBA LA MAFUTA TANGA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni