Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo
ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Oparesheni UKUTA yaliyokuwa yamepangwa
kufanyika kesho nchi nzima.
Mbowe ametoa kauli hiyo ya kuahirisha maandamano mchana huu wakati akiongea na
vyombo mbalimbali vya habari.
Amesema sababu kubwa za kuahirisha maandamano hayo ni busara za viongozi wa
dini ambao wameiomba Chadema iwape muda wa kutafuta Suluhu
Mbowe amesema maandamano hayo yameahirishwa hadi Oktoba Mosi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni