Leo August 25 2016 Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Andrew Wilson
Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kabla ya uteuzi huo Andrew
Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu
Tanzania (BOT).
Pia Andrew Wilson Massawe amechukua
nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe
unaanza mara moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni