Jumatano, 17 Agosti 2016

MUHONGO , BENK YA DUNIA FURSA ZA MAENDELEO NI KWENU, UMEME SASA SIO KIKWAZO.



WAZIRI WA NISHATI MADINI SOSPETER MUHONGO AKIFUNGUA
MRADI WA UMEME VIJIJINI (TREEP) WA AWAMU YA PILI KIJIJI CHA KWEDIZINGA KATA YA KABUKU WILAYA YA HANDENI 
WAZIRI wa Nishati na Madini, Sospeter Mohongo, amewataka wakulima wa mbogamboga na matunda vijijini kuitumia fursa ya ujio wa umeme vijijini wa Rea kwa kufungua miradi na viwanda vidogovidogo.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini (TREEP) awamu ya pili kijiji cha Kwedizinga kata ya Kabuku Wilayani Handeni kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, Muhongo alisema Serikali inataka kila mwananchi kutumia nishati ya umeme majumbani.

Alisema wananchi vijijini wako na fursa nyingi za maendeleo laikini wamekuwa duni kutokana nna kutokuwa na nishati ya umeme hivyo kuwataka kuhakikisha wanafunga umeme majumbani kwao.

“Hapana shaka kuwa wananchi wa vijijini ni matajiri lakini utajiri wao hauonekani na badala yake wenye pesa huwatishia mazao yao kununua kwa bei ya hasara kutokana na kutokuwa na umeme” alisema Muhongo na kuongeza

“Mahindi na mpunga wenu mutakoboa hapa hapa na sio tena mjini, wanunuzi watakuja kwenu na kuwauzia kwa bei munayotaka nyinyi tofauti na sasa ambapo hamuna umeme na kulazimika kuwauzia kwa bei ya hasara” alisema.

Aliwaka wananchi hao kuhakikisha awamu ya pili ya usambazaji umeme vijijini wananchi haiwapiti hivyo kutaka wenye mifugo na rasilimali yoyote kuuza na kupata pesa za kulipia umeme huo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Bank ya Dunia, Bella Bard, alisema anajua umuhimu wa nishati ya umeme majumbani na kuona ili kuondosha umasikini ;lazima umeme uwepo.

Alisema Bank ya Dunia inatambua kuwa vijijini ziko fursa nyingi za maendeleo lakini kikwazo kikubwa ni umeme hivyo kwa ujio huo nikuwataka kila mmoja anakamilisha taratibu za kufungiwa.

“Tunatambua kuwa umasikini uko mjini na sio vijijini ambako umasikini wao ni kutokana na kutokuwa na umeme tu, hii kwa kweli ni changamoto  ambayo tumeigundua na ndio maana nguvu za Serikali na bank ya dunia imejikita kusambaza vijijini” alisema Bard.

Aliwataka wananchi waishio karibu na nyya za umeme ulipopita kuhakikisha inailinda miundombinu yake pamoja na kuzuia hujuma yoyote ambayo itaathiri mradi huo wa usambazaji umeme vijijini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni