Walengwa wa ruzuku ya kusaidia kaya masikini wakihakikiwa tayari kwa kupokea ruzuku kutoka Tasaf katika Kata ya Chumbageni Mtaa wa Kisosora Jijini Tanga
Wanufaika wa mpango wa kusaidia Kaya Masikini Halmashauri ya Jiji la Tanga wa Kata ya Chongoleani.
Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Halmashauri ya Jiji la Tanga Kata ya Mpirani .
Mratibu wa Tasaf Jiji la Tanga Juma Mkombozi akitoa ufafanuzi wa mpango huu wa kunusuru Kaya Masikini unaofanya na Tasaf, amesema kaya Masikini 5,422 na Mitaa 88 ya Jiji la Tanga kwa walengwa wanatarajia kupokea ruzuku ambayo imeanza kugawiwa tarehe 3 hadi tarehe 10 Mwezi Agasti.
Mkombozi alisema ruzuku hii inayo tolewa ni ya mwezi Julai, Agosti kwa walengwa wa mpango wa ruzuku ya Msingi na ruzuku ya kutimiza Masharti ambayo upewa kaya yenye walegwa wanaotakiwa kutimiza Masharti ya Elimu na Afya.
Pia Mratibu alisema hii ni mara ya saba kwa Tasaf kutoa ruzuku hii kwa kaya masikini na kuwataka walengwa kuzitumia Pesa hizi katika Malengo ya Mradi na sio kufanyia vitu visivyo na msingi.
"Mkombozi alisema hela hizi sio nyingi lakini Serikali ina lengo la kusaidia jamii kupunguza ukali wa maisha magumu"
Alisema wapo watu wengine wameweza kujikwamua kiuchumi kutoka katika hali duni sana na kufikia hali ya hafadhari hivyo amewataka walegwa wote kuzitumia hela kwa kujikwamua na kuwasaidia familia kielimu na kiafya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni