Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake) wakiwapungia
wananchi wa Mpanda wakati walipowasili kwenye uwanja wa Kashaulili mjini
Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka
watendaji wa halmashauri mkoani Katavi kuwa makini na matumizi ya fedha za
maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao na atakayethubutu kuzichezea
zitamuunguza.
“Fedha
hii tafadhali ni ya moto. Msicheze na hii ya halmashauri tunayoileta hapa
halmashauri kwa ajili ya wananchi itawakunguza vidole. Tunaileta kwa madhumini,
tunataka wananchi wahudumiwe,“ alisema.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Agosti 21, 2016) wakati akihutubia
umati mkubwa wa wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja
cha Azimio wilayani Mpanda.
Alisema
Serikali imeanza kupeleka fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri
mbalimbali hivyo ni vema kila mtendaji ahakikishe fedha hizo zinatumika kwa
ajili ya ujenzi wa miradi iliyokusudiwa na si vinginevyo.
Waziri
Mkuu alisema ni lazima wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri
wahakikisha viwango vya ubora wa miradi inayojengwa katika maeneo yao kuwa
inalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu kwenda wilayani Mpanda na kuangalia namna ya kuipanua
hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambayo inahudumia mkoa wote wa Katavi.
Alisema
hospitali hiyo ilijengwa mwaka 1957 kama zahanati ambayo kwa sasa yanatumika
katika kuwahudumia wananchi wate wa mkoa huo imezidiwa hivyo alimuagiza mkuu wa
mkoa huo Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga kuharakisha ujenzi wa hospitali
ya mkoa.
Aidha,
Waziri Mkuu alisema kuwa wakati mkoa ukiwa kwenye harakati za ujenzi wa
hospitali ya mkoa wilaya nazo zianze ujenzi wa hospitali za wilaya ili
kuhakikisha sera ya Serikali ya kuwa na hospitali katika kila wilaya
inatekelezwa.
Alisema
kwa sasa madaktari na wauguzi wanaofanya kazi kwenye hospitali ya Manispaa ya
Mpanda wamezidiwa kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa kuliko uwezo
wao.
Hata hivyo
Majaliwa amewataka madaktari na wauguzi wa wilaya ya Mpanda kuendelea kufanya
kazi kwa kushirikiana na wenzao wa Manispaa.
Awali
hospitali hiyo ilikuwa chini ya uongozi wa halmashauri ya Mpanda. Hospitali
hiyo kwa sasa ipo chini ya Manispaa ya Mpanda hivyo Waziri Mkuu ameutaka
uongozi wa mkoa huo kuboresha huduma kwa kupeleka dawa na vifaa tiba
vitakavyoweza hospitali hiyo kuhudumia wagonjwa wa mkoa.
Mkoa
umetenga sh. bilioni 1.7 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya mkoa.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni