Jumamosi, 30 Julai 2016

WATUMISHI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI WACHANGIA DAMU SALAMA



Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias  Andengenye akihutubia Maafisa, Askari na watumishi wote wa  Jeshi hilo wakati akifungua zoezi la uchangiaji damu salama ambalo lilishirikisha vituo vyote vya Zimamoto mikoani, ufunguzi huo ulifanyika katika viwanjwa vya Zimamoto na uokoaji mkoa wa Ilala.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias  Andengenye akichangia damu katika zoezi lililofanyika viwanja vya kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala zoezi lililoshirikisha vituo vyote vya Zimamoto mkoa wa Dar es Salaam.

Maafisa, Askari na watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka katika vituo vya Zimamoto Makao Makuu, Chuo, Ilala, Kinondoni, Temeke na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakimsikiliza Kamishna Jenerali wakati akihutubia katika ufunguzi wa zoezi la uchangiaji Damu salama lililofanyika katika viwanja vya Zimamoto mkoa wa Ilala.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amewaongoza viongozi waandamizi, maafisa, askari na watumishi wote wa jeshi hilo katika zoezi la uchangiaji damu salama ili kutimiza dhima ya kuokoa maisha ya watu wanaopoteza maisha kwa ajali za moto, ajali za barabarani, vifo vya mama wajawazito wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua na magonjwa mbalimbali kama vile ukimwi, malaria, anaemia na kansa.
 
Zoezi hili limefanyika katika viwanja vya kituo cha jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa ilala  kwa kushirikiana na taasisi ya mpango wa damu salama ulio chini ya wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia watoto na wazee.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni