WAZIRI wa
Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki,
ameliagiza Jeshi la Polisi na Vyombo vya Usalama kuwafichua watumishi hewa na
wenye vyeti feki.
Akizungumza na
wakuu wa Idara na watumishi mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Umma jana,
Kairuki alisema mbali ya kupewa taarifa ya kuwepo kwa watumishi hewa Tanga 198
amedai anaamini wapo wengi.
Alisema ili
kuweza kuwafichua ameliomba jeshi la polisi na vyombo vya usalama kusaidia ili kuwakamata
na kuwapeleka katika vyombo vya sheria kabla ya wao kujinasua.
“Ninaomba
jeshi la polisi na vyombo vya usalama kusaidia kuwafichua watumishi hewa na
wenye vyeti feki, tunaamini tutawakamata na kuwapeleka mahakamani kabla ya wao kujinasua”
“Tunatambua kuna
watumishi wenye dhamana ambao hawana sifa ila kwa kuwa na vyeti vyao feki
wamejipatia vyeo ambavyo wanashindwa kuongoza” alisema Kairuki
Pia, Kairuki alizungumzia
kuhusu maadili nakusema watumishi wanatakiwa kuzingatia maadili ya kazi na
kutunza siri za Serikali na kusema kuwa yoyote ambaye atashindwa ni vyema
kujiengua mapema.
Alisema Wizara
yake itahakikisha kila mtumishi na mkuu wa Idara anaitumia vyema nafasi yake
kwa kuwahudumia wananchi kwa usawa bila ubaguzi ili kuondosha manung’uniko
kutoka kwa wananchi.
Alisema kuna
baadhi ya Idara zimekuwa zikilalamikiwa kwa kushindwa kuleta uadilifu na usawa
kwa utoaji wa huduma hivyo kuagiza tabia hiyo kukomeshwa mara moja.
Alisema mkuu
yoyote wa Idara ambaye atashindwa
kuitumia nafasi yake kwa uadilifu
ajiengue mwenyewe kabla ya fagio kumpitia kwa madai kuwa Serikali ya awamu ya
tano haitakiwa watumishi kufanya kazi kwa mazoea.
Waziri Kairuki
aliwataka wananchi kutoa taarifa za malalamiko katika Idara za Serikali na za
Umma ili kukomesha ukiritimba na manyanyaso na
utoaji wa huduma kwa upendeleo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni