Licha ya uwepo Wa tatizo la utumikishwaji wa watoto hapa nchini bado hakuna tafiti za kina zilizofanyika ili kuweza kubaini ukubwa Wa tatizo hilo Kwa sasa.
Hayo yamesemwa na Mhadhiri kutoka chuo kikuu huria cha Tanzania OUT Ladislaus Fredrick Wakati Wa semina Kwa wajumbe Wa kamati za kutokomeza utumikishwaji Wa watoto wilaya ya Tanga.
Ladislaus Fredrick alisema mpaka sasa tatizo utumikishwaji wa watoto hapa nchini bado halijafanyiwa utafiti Wa kutosha ili kuweza kubaini ukubwa Wa tatizo pamoja naathari zake.
"Kwa utafiti mdogo tu unaonyesa Mikoa ya Tanga na Kigoma ndio inaongoza Kwa kuwa na watoto wengi wanaotumikishwa katika ajira zisizo rasmi lakini bila takwimu sahihi hatuwezi kujua ukubwa Wa tatizo hilo"alisema Fredrick.
Aliongeza kuwa licha ya kuwepo Kwa mikakati ikiwemo uwepo wa sheria za kudhibiti pamoja na mikakati lakini bado watoto wameendeea kuwa wahanga Wa ajira zisizo rasmi hapa nchini.
Kwa upande wake Mratibu Wa mradi Wa WEKEZA Mkoa Wa Tanga Theresa Fovo alisema kuwa mradi huo umelenga kuhakikisha unatoa elimu Kwa jamii kuhusu kukomeshwa pamoja madhara ya ajira Kwa watoto.
Alisema kuwa kupitia kumuwezesha mtoto kielimu ndio pekee itakuwa ni mkombozi Wa ajira Kwa watoto katika maeneo mbalimbali husisani Vijijini.
“Theresa Fovo alisema mpaka sasa wamefanikiwa kufungua Club
za watoto
katika mashule wilayani Tanga, Muheza, na Korogwe ili kufwatilia na
kutoa takwimu mashuleni na zaidi ya watoto
4,000 wamefikiwa na kaya 1,680 na vijana 2,100 wameweza kunufaika na mradi wa
WEKEZA.
Pia washirika Semina walishukuru kwa mafunzo mazuri
ambayo wameyapata
yatasaidia sana katika kuelimisha jamii kupiga vita utumikishwaji wa
watoto kwani tatizo hili ni kubwa katika jamii na pia jamii haina elimu ya
kujua swala la utumikishwaji mtoto ni kosa kisheria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni