Jumatano, 6 Julai 2016

MCHUNGAJI IDANI KAMOTE AWATAKA WANAWAKE NA WASICHANA WA JIJI LA TANGA KUDUMISHA MAVAZI YA KITANZANIA.



Wanawake na mabinti jijini Tanga wametakiwa kuvaa mavazi yanayozingatia maadili ya kitanzania pindi wanapohudhuria katika nyumba za ibada.

Hayo yalisemwa na mchungaji wa kanisa la anglikana chumbageni jijini Tanga mchungaji Idani Peter Kamote wakati wa majojiano maalum na mwandishi wetu katika ofisi zake mapema leo.

Mchungaji Kamote alifafanua kwamba ukosefu wa maadili umesababisha wanawake kuiga tamduni za uvaaji kutoka nchi nyengine ,utandawazi na uhuru wa kupitiliza kutoka kwa wazazi hali ambayo hupelekea mmomonyoko wa maadili ya Makanisa.

Hata hivyo wazazi waliomba ushirikiano kutoka kwa viongozi wa dini ili kuondoa tatizo hilo kwa upande wa baadhi ya wanawake mmoja wa wazazi hao Bi Dorith Mavoa alisema iwekwe sheria maalumu ya mavazi katika nyumba za ibada ilikukabiliana na changamoto hizo.

Kwa upande wao mabinti walisema tatizo hilo husababishwa na utandawazi pia huamua kuvaa mavazi hayo ili kuendana na wakati mmoja wa mabinti hao Aneth Joseph alisema yeye huvaa mavazi aina hiyo ili kuendana na dunia ya leo.

Mchungaji Kamote aliwataka wazazi kuwalea watoto wa kike katika nyendo njema ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha juu ya hekima na heshima swala la uvaaji ili kuponya kizazi hiki na kijacho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni