Jumanne, 19 Julai 2016

NAIBU WAZIRI WA NYUMBA NA MAKAZI AWAONYA WAKUU WA IDARA KUACHA TABIA YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI MAOFISINI TANGA.



NAIBU Waziri wa Nyumba na Makazi, Angelina Mabula, amewagiza wakuu wa Idara na Taasisi za Serikali kuacha mazoea ya kutatua migogoro wakiwa maofisini na kuwaagiza kuwa tabia hiyo ikomeshwe mara moja.

Akizungumza na viongozi mbalimbali Idara ya Mipango miji na Shirika la Nyumba la Taifa, Mabula alisema kuna baadhi ya wakuu wa Idara wameshindwa kubeba dhamana ya kuwahudumia wananchi na kujikalia maofisni.

Pia alisema tabia ya kutatua migogoro ya wananchi wakiwa ofisini ikomeshwe na kuwataka wakuu hao kufuatilia kero za wananchi sehemu husika.

Akizungumzia baadhi ya watendaji kujipangia  kazi na kuomba pesa za ziada, Mabula alisema tabia hiyo iachwe na kila mtu afanya kazi kwakujitoa  na kuwahudumia wananchi kikamilifu.

Alisema kuna baadhi ya watendaji wamekuwa wakijipangia kazi baada ya muda kutoka maofisini na kujilipa pesa jambo ambalo amesema hataki kulisikia tena.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni