Jumatano, 20 Julai 2016

UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA WAPOKELEWA VIZURI NA WANANCHI MKOANI TANGA.



Wananchi wa mtaa wa Putini kata ya Chongoleani Jijini Tanga wameiomba Halimashauri ya Jiji  kuwatafutia eneo jipya la kujenga shule ilikupisha eneo linalotarajiwa kujengwa matanki ya kuhifadhia mafuta wakati wa utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta.

Hayo yalisemwa na baadhi ya wakazi wa kata hiyo wakati wakiongea na waandishi wa habari walisema baada ya tathimini waliweza kugundua shule hiyo ipo ndani ya eneo la mradi huo.

Walisema kuwa shule hiyo ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi kwa lengo la kuwapunguzia kutembea umbali mrefu wanafunzi wanaoishi katika mtaa huo.

Naye  Saleh Gofa alisema kuwa ni vema Jiji wakawaonyesha eneo jingine la kujenga shule kabla ya mradi haujaanza kutekelezwa katika eneo hilo.

“Tunaiomba Halmashauri ya Jiji itutafutie eneo jingine na kama kunauwezekano wa kujengewa shule nyingine itakuwa vizuri zaidi kwani ya awali ilitokana na nguvu za wananchi wenyewe”alisema Gofa.

Markus Tuwaya ameiomba Halmashauri kuwasaidia kuwatafutia maeneo mengine ya makazi kwani kuna baadhi ya nyumba zitabomolewa ili kupisha mradi pamoja na fidia ili waweze kuanza maisha mpya tena bila ya kusuasua.

“Kunatabia imejengeka ikiwa wananchi wanalipwa fidia bila ya kuonyeshwa maeneo mengine ya kuendeleza makazi tunapo hamia wananchi wanatuuzia maeneo kwa gharama kubwa zaidi “alisema Tuwaya.

Hata Hivyo Mwenyekiti wa Mtaa huo Said Kanuni alisema kuwa tayari taarifa za uwepo wa wananchi wanaohitaji fidia ameshaziwasilisha kwa Mkurungenzi wa Jiji Daudi Mayeji kwa ajili ya taratibu nyingine.

“Changamoto kubwa ni baadhi ya wananchi hawana taarifa za kutosha kuhusu mfumo wa fidia watakao lipwa hivyo husababisha kuwa na hofu ya kukosa fidia kabisa”alisema Kanuni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni