Ujenzi wa kivuko kipya cha Mv
Pangani uko katika hatua za mwisho na kinategemea kumamilika Julai mwaka huu na
kuanza kutoa huduma.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi. Lekujan Manase alipotembelea na
kukagua mradi wa ujenzi wa kivuko hicho ambao upo mbioni kukamilika kwa kuanza
kutoa huduma kwa wananchi.
“Kivuko hiki kipo katika hatua za
mwisho za ujenzi wake na leo tumekuja hapa kukagua mitambo ya kuendeshea kivuko
(propulsion units) pamoja na injini zilizofungwa katika kivuko hiki ili
kukamilisha ujenzi wake na hatimaye kianze kufanya kazi” alisema Mhandisi
Manase.
Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka
Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme kutoka Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Dkt. William Nshama alieleza kuwa ameridhishwa na kasi ya
ujenzi wa kivuko hicho unaofanywa kwa kiwango cha kimataifa na kuwa kivuko cha
Mv Pangani kinatarajiwa kutoa huduma kati ya Pangani na Bweni Mkoani Tanga
baada ya ujenzi wake kukamilika.
Kwa mujibu wa kampuni ya Songoro
Marine Transport LTD kivuko hicho kina uwezo wa kubeba magari sita na abiria
100 kwa pamoja, na ni sawa na uzito wa tani 50.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni