Wito umetolewa kwa wakristu
wote nchini kujitoa kwa hali na mali kuwasaidia
wenye mahitaji ili waonje neema
ya kuishi hapa duniani na mwisho kufurahia maisha ya milele mbinguni.
Rai hiyo imetolewa na
mkurugenzi wa mashirika ya kipapa na paroko wa parokia ya mtakatifu Anthoni wa
Padua chumbageni kanisa kuu jimbo katoliki la Tanga, kwenye adhimisho la ibada
ya misa takatifu ya dominica 15 ya mwaka c parokiani hapo alisema kila mtu kwa
nafasi yake aoneshe ukarimu wake kwa kuwasaidia wahitaji mbalimbali kama vile
wajane ambao wanakosa haki zao za msingi.
“kumekuwa na wimbi kubwa la
wakosa haki zao za msingi hasa wajane wanadhurumiwa ambapo wanakosa watetezi
wakiwa wanadai haki zao, wakienda Makamani kutafuta msaada wa kisheria na
ukizingatia wapo wasimamizi wakristo wanaoshindwa kutoa msaada na kulinda wale
wanao dai haki katika eneo hilo”.alisema Padre Semng’indo.
Hata hivyo Padre huyo aliwataka
Kila mtu atambue kuwa Kristu alitenda haki bila kubagua mtu basi kwa nafasi ya
watumishi kwa ngazi walizo nazo wasaidie haki na mahitaji kupatikana kwa usawa
bila kuwepo manung’uniko kwa kuyafanya hayo itazidisha upendo na umoja katika
maisha ya wanadamu ambaye anasafiri hapa kuelekea mbinguni.
“Kumekuwa na tabia kwa
baadhi ya huduma katika jamii kwa mfano eneo huduma ya afya wapo baadhi ya
watumishi wanashindwa kutoa huduma husika kwa kudai chochote kitu huku wakishindwa
kusima maadili ya kazi na kushindwa kutambua kuwa wamepewa karama hiyo
ilikutimiza mapenzi ya Mungu kwa kutoa huduma kwa wahitaji.”alisema Padre Semng’indo.
Sambamba na hayo Padre Semngindo
alikemea tabia ya watu kuzalilisha utu wa mwanadamu pale ajari au tukio na
maafa yanapo tokea watu wanashindwa kutoa msaada kwa haraka kwa kuokoa maisha
ya wale waliyo fikwa na matatizo badala ya kutoa huduma wao wanatumia simu zao kwa kupiga picha au
kurekodi tukio zima na kurusha kwenye mitandao ya kijamii kufanya hivyo sio
jambo la msingi kwa kutupia tukio hilo akijiona ni wakwaza kwa kufanya hivyo akumpendezi
Mungu kwani Mungu wetu anatufundisha katka ule mfano wa Msamalia mwema ambaye
alitoa msaada wa mtu aliye fikwa na matatizo ya kupigwa na wanyang’anyi.
“Wewe ukitupia matukio ya
ajari katika mitandao huku ukiwa unauwezo wa kutoa msaada wa haraka kwa Waathirika
wa tukio unapata faida gani, ni bora kutimiza matendo ya huduma ya kimungu kwa kuwasaidia
wale wote wanafikwa na matatizo kwa kufanya hiyo utaonesha upendo kwa mungu na
wanadamu kwa kutekeleza msaada wa wahitaji, basi msichanganyikiwe na mitandao
ya kijamii ambayo imeshika kasi kwa sasa kwani aitatufikishi mbinguni”. alisema
Padre Semng’indo.
Pia Padre huyo alitumia
nafasi hiyo kuwakumbusha Wakristu kuwa mwaka huu ni mwaka wa huruma ya Mungu
tuishi kwa maneno na matendo wenye huruma kwa watu wa aina zote ili kazi ya Mungu
ionekane kwa watu wote kama vile salamu ya jubilee ya mwaka wa huruma ya Mungu
inavyo sema ‘iweni na huruma kama baba yenu wa mbinguni alivyo na huruma’ na
kuwa mfano wa kweli kama Yule msamalia mwema alivyo msaidia myahudi aliye pigwa
na wanyang’anyi bila kujali macho ya watu au maneno akatoa msaada na kumpendeza
Mungu kwa nafasi yake, ukitoa msaada kwa watu wote bila kuangalia wewe kabila
gani ama rangi gani toa msaada tu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni