Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakati akikagua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Wilayani Mkinga wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Yona Maki (mwenye tai) na Meneja NHC Tanga Issaya Mshamba.
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Tanga.
Baadhi ya Nyumba za
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Wilayani Mkinga ambazo Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ameamuru
watumishi wa wilaya hiyo waamie ifikapo tarehe 1 Agosti 2016.
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula
akiongea na wananchi wa Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga na kutolea ufumbuzi
migogoro ya Ardhi inayowakabili
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (mwenye tai nyekundu) mara baada ya kujadili changamoto za ardhi katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula ametoa Siku kumi na mbili kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuhama Tanga Mjini na kuhamia Wilayani Mkinga mahali zilipo nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizojengwa kwa ajili yao.
Naibu Waziri Mabula ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake wilayani Mkinga ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kutembelea eneo zilipojengwa nyumba hizo na kumuagiza Meneja wa NHC mkoa wa Tanga kuhakikisha tarehe 1 mwezi wa Agosti 2016 watumishi hao wanahamia katika nyumba hizo.
kwa sasa watumishi hao wamekuwa wakiishi Tanga mjini na kufanya kazi wilayani mkinga, hali inayowalazimu kusafiri zaidi ya kilometa 50 kilasiku kwenda na kurudi.
Mheshimiwa Mabula yupo katika ziara ya siku nne mkoani Tanga ambapo ametembelea Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya za Tanga mjini, Korogwe pamoja na kuzindua baraza jipya la Wilaya ya Kilindi. Hata hivyo mbali na mabaraza ya Ardhi mheshimiwa Naibu Waziri anatembelea miradi ya NHC pamoja na kutatua kero za migogoro ya Ardhi na changamoto za watumishi wa sekta za Ardhi mkoani Tanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni