Ni tukio la
kusikitisha baada ya Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Mbuguni wilayani Arumeru
jijini ARUSHA, Paulina Mafembo na wagonjwa watano wanadaiwa kutekwa na watu
wanaodhaniwa kuwa ni vibaka kisha kupelekwa porini kwa nia ya kuwabaka.
Tukio hilo lilitokea
hivi karibuni baada ya mtu mmoja kufika katika kituo hicho majira ya saa 10
usiku na kudai kuwa anaumwa na alipofunguliwa ili apatiwe matibabu ndipo watu
wengine wanne wakavamia na kuanza kuwapora wajawazito vitu vyao.
Akizungumzia
na Amani, Paulina ambaye amenusurika kubakwa alisema baada ya
kumfungulia mtu huyo alishangaa kuona wengine wanne wakivamia wakiwa na mapanga
na kuanza kuwapokonya wajawazito kila kitu walichokuwa nacho.
“Baada ya hapo
walianza kuwabeba wagonjwa ambao ni akina mama na kutokomea nao gizani na
kuanza kuwafanyia vitendo vya ubakaji. Na mimi pia nilishikiwa panga na
kuamriwa kuvua nguo, nilikubali, yule kibaka alifanya kosa la kuweka panga
chini ndipo nikapata mwanya wa kukimbia,” alisema Paulina.
Naye Mwenyekiti wa
Kijiji cha Mbuguni, Wilbard Mungure alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema kuwa walishatoa taarifa kwa jeshi la polisi na hatua za kuwasaka
watuhumiwa zinaendelea.
Kwa upande wa
Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi na hakuna
mtu anayeshikiliwa kwa tukio hilo.
GPL(P.T)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni